Mgodi wa GGM na Wanawake wa Geita

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nyankumbu wakijisomea library. Shule hii ya wasichana ni ya mfumo wa sayansi na inawanafunzi zaidi ya 900, imesheheni vifaa vya maabara, nyumba za kisasa 36 kwa ajili ya waalimu, madarasa 21 na viwanja mbalimbali vya michezo. Pamoja na miradi mingine ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, GGM imewekeza shilingi Bilioni 10 katika ujenzi wa shule hii kubwa na ya kisasa. 
Wanawake wakiwa wanashona na kutaririzi katika mradi chini ya mradi mkubwa uitwao Geita Economic Development Project (GEDP) mradi huu umelenga kuwawezesha wanawake na jamii ya Geita katika kujiinua kiuchumi na unahusisha miradi ya kilimo cha mpunga na alizeti, Kushona na kutarizi, ufyatuaji matofali, Welding na ushonaji na kutengeneza viatu .

Kwa kuzingatia mchango wa wanawake katika Jamii ya Geita, Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) umeweza kufanya miradi mbalimbali ambayo imelenga kuwawezesha wanawake katika kujinyanyua kiuchumi, kijamii na kielimu. GGM inajivunia katika kuleta chahu ya maendeleo kwa akina mama ambao ni nguzo la taifa la Tanzania na duni yote.
Shule ya Bweni ya Wasichana Nyankumbu 

Hii ni shule kubwa yenye madarasa 21 na uwezo wa wanafunzi 900. Shule ni ya mchipuko wa sayansi na ni shule ya bweni. GGM imewekeza shs. Billion 10 katika mradi huu ambapo una vifaa vya kisasa vya sayansi kwenye maabara ya fizikia, kemistry na baiolojia vilevile vifaa vya maabara ya somo la komputa, nyumba za walimu 36 viwanja vya michezo, maji na ukuta wa kuzunguka eneo lote la shule.

Lengo la mradi huu ni kuhakikisha wasichana wanapata  kiwango kikubwa cha elimu hususani wasichana kutoka katika jamii ya Geita na hivyo kujenga mazingira salama, na kuongeza nafasi ya wasichana kupata mafanikio ya kitaaluma na maendeleo ya jamii inayozunguka na Taifa zima.
Faida kwa Jamii: 

Wasichana zaidi ya 900 watakuwa wanasoma katika shule hii kila mwaka. Mabweni yatapunguza hatari ya usalama itokanayo na wasichana kutembea umbali mrefu kwenda na kutoka shule. Vile vile itawapa wasichana wadogo fursa ya kuzingatia masomo yao na mafanikio ya kitaaluma, na kujenga fursa za uongozi, ambapo itakuwa na faida kwao, familia zao, na jamii inayowazunguka. Mradi huu pia utawapa wasichana wa Geita fursa ya kushindana na wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali nchini kwenye mazingira mazuri. Hii itaipatia nchi ya Tanzania wananchi wema wenye kuchangia katika maendeleo ya jamii na taifa lao kwa ujumla.
Mradi wa Maji

Mradi wa Usambazaji Maji Geita unasambaza maji safi ya kunywa kwa wakazi zaidi ya 130,000 wa Geita. Hii ni historia kwa huduma ya maji na afya kwa jamii ya Geita. Umuhimu wa mradi huu wa maji katika kubadilisha maisha ya wakazi wa mji huu unaokua ni muhimu mno. Wanawake na wasichana hawahitaji kwenda umbali mrefu kuchota maji, hivyo kuepukana na hatari za kubakwa katika vichaka na hivyo kutimiza malengo ya kazi nyingine za nyumbani au shule. Mradi huu unakwenda sawa na vipaumbele vya serikali ya awamu ya Tano katika kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa maji katika jamii zetu za Tanzania.

Mradi wa Kuzuia Malaria kwa Akina Mama - wanawake na wajawazito
Mradi huu kwa kuanzia ulikuwa unafanyika kwenye kata mbili yaani Kalangalala na Mtakuja, ambazo ziko katika mji wa Geita. Hata hivyo kutokana na mabadiliko ya kiutawala mradi huu sasa unahusisha jumla ya kata sita.  Mradi unawafikia na kuwanufaisha zaidi ya watu   100,000 waishio kwenye kata zinazohusika. Miongoni mwa wanufaika hao wamo watoto 17, 800 walio chini ya umri wa miaka mitano (5) na wanawake wajawazito - makundi haya mawili ndio waathirika wakubwa wa malaria hapa nchini.
Zaidi ya vijana 200 kutoka Geita wamepata ujuzi na ajira za muda wakati wa kutekeleza mradi, na hivyo kuwaongezea thamani katika maisha yao. Matukio ya malaria kwenye eneo la mradi yamepungua kutoka 3000 mwaka 2006/7 hadi kufikia 138 mwaka 2013. Haya ni mafanikio makubwa katika kukabiliana na magonjwa na vifo hasa vya watoto na akina mama wajawazito. Kwa ushirikiano na Halmashauri ya wilaya ya Geita, GGM imesaidia ujenzi wa Kituo cha Mradi wa Malaria Geita.. Programu hii imewawezesha watu zaidi ya 100,000 kupata kinga dhidi ya maambukizi na kusaidia lengo letu la kuwekeza kwenye afya ya nguvu kazi ya migodi na watu wa jamii inayotuzunguka. Kumekuwa na ongezeko katika uwezo wa kamati ya Usimamizi wa Afya ya Wilaya ya Geita kwa njia ya mafunzo na kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa mradi. Hii imefanya ushirikiano kati ya sekta ya umma na ile ya binafsi kuwa njia bora ya kusaidia mradi kuwa endelevu.

Msaada wa Ambulance na Zahanati ya Nyakabale: 
GGM imetoa msaada wa ambulance 3 kwa wakazi wa vijiji vya bukoli na Nzera
Gari hizi za aina ya Landcruizer zenye thamani ya milioni 40 kila moja, zinasaidia kusafirisha wanawake wajawazito kunapokuwa na hitilafu katika uzazi. Hivyo wanawahishwa kwenye hosipitali kubwa kama Bugando  na kupunguza vifo vya watoto na wajawazito, lakini pia ni msaada mkubwa kwa wagonjwa waliozidiwa kwa malaria na magonjwa mengine.
Zahanati ya Nyakabale iliyojengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi million330, ina nyumba za watumishi, mtambo wa umeme wa jua na kisima cha maji ili kusaidia wakazi wa Nyakabale hususana wanawake na watoto kupata huduma za Afya karibu na makazi yao.

Ajira kupitia Mradi wa Ushonaji na Kutarizi na kilimo.
GGM kwa kushirikiana na Halmashauri ya mji wa Geita, imefanikiwa kuwekeza katika ununuzi wa mashine za kushona na kutarizi , mashine za kisasa zinazotumia kompyuta, ambapo wanawake wa Geita wameweza kujipatia ajira na ujuzi.
Mradi huu unakwenda sambamba na mradi wa kilimo cha mpunga na alizeti ambapo zaidiya kaya elfu nne zinanufaika moja kwa moja na mradi. Zaidi ya Heka 900 zinalimwa mpunga na alizeti hivyo kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa chakula cha kutosha lakini lengo kubwa ni kilimo cha biashara hivyo kuwezesha wanawake wa Geita kujinyanyua kiuchumi pamoja na familia zao.

Ukarabati wa hospitali Kuu ya Mkoa wa Geita na ujenzi wa Vituo vya Afya 
Kwa kujali afya za wanawake katika mkoa wa Geita, GGM ikishirikiana na Halmashauri na uongozi wa Mkoa wa Geita, imekarabati hospitali kuu ya mkoa ambayo ina zaidi ya miaka 50 toka ilipojengwa.
GGM imenunua vifaa mbalimbali vya kisasa ikiwapo vifaa vya magonjwa ya moyo, meno nk. Kwa sasa wagonjwa waliohitaji kusafiri kwenda Moi hospital, Dar esalaam, hawahitaji tena kufanya hivyo kwani vifaa na madaktari wanapatikana hapo Geita. Ukarabati huu unapelekana na ujenzi wa vituo vya afya vya Nyakabale, bukoli na kituo cha ushauri na upimaji ukimwi – VCT geita mjini.
Pamoja na miradi mingineyo ambayo inanufaisha wanajamii wote wa Geita, GGM tunajivunia kwa uwekezaji huu ambao unathibitisha namna ambayo mgodi wa GGM unatoa kipaumbele kwa jamii lakini pia unazingatia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wanawake wanaouzunguka” Alisema Tenga Tenga, Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano wa Mgodi.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.