NA MWANDISHI WETU;
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji,
Prof Zakalia Mganilwa amewataka umoja wa wanake katika chuo hicho UWANIT kuwa wabunifu ili waweze kuendesha umoja wao bila
kutegemea wahisani, akisisitiza kuwa kama wasipokuwa wamoja na wabunifu chombo
hicho kinaweza kukosa pesa na mwisho wake unaweza kuwa mbaya.
Wito huo ameutoa
katikati ya wiki wakati akizindua kwa mara ya kwanza umoja wa wanawake wa chuo
hicho (UWANIT) katika Hotel ya GM elegance iliyopo Sinza Jijini Daresalaam.
Prof Mganilwa
amesema ameshuhudia umoja wa namna hiyo unavyokufa kwa kukosa pesa,lakini hataki
kuona hilo likitokea kwa umoja wa UWANIT kwani anaamini wanaweza kubuni miradi
mbalimbali ya kuwaingizia kipato na kwa kuwa kinamama ndio watumiaji wazuri wa
mitandao ya kijamii wataitumia mitandao hiyo kutangaza shughuli zao za kibunifu
jambo likalowafanya kufika mbali.
“Duniani kote
Mwanamke ni nguzo muhimu katika malezi ya familia nami naamini kupitia umoja
huu mtakua walezi wazuri wa Chuo chetu hasa ukizingatia hii ni Taasisi ya Elimu
ambayo inalea wanafunzi walio katika kipndi cha kushawishika kirahisi,hivyo
kupitia umoja huu wekeni utaratibu utakaoweza kusaidia wanachama kujikwamua
kiuchumi,kitaaluma lakini pia mkumbuke namna ambavyo mnaweza kuwainua hata
wanafunzi wetu wale wenye skills mbalimbali ili kuwaandaa kuwa walezi bora.”
Alisema Prof Mganilwa
…AKUBALI OMBI LA KUWA
MLEZI WA UMOJA WA UWANIT
Katika hatua
nyingine Mkuu huyo wa Chuo amekubali kwa mikono miwili ombi la kuwa Mlezi wa
Umoja huo, na kwamba yuko tayari kutoa msaada wowote ikiwemo ushauri na hata
mengineyo kwani anaamini umoja huo ni mzuri kwa mustakabali wa maendeleo ya
chuo.
“Nimesoma malengo
yenu, kwa kweli ni mazuri na yamelenga kukisaidia Chuo kusonga mbele,
nimefurahishwa sana na jambo hili niwaahidi Full support yangu; naamini
mkifanikiwa nyie itakuwa faraja kwa Jumuiya nzima ya NIT” aliongeza
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake NIT (UWANIT) Bi Joyce Bakari Mpunga akizungumza na wadau walioshiriki katika uzinduzi huo. katika umoja huo una jumla ya wanachama 96,
|
Awali akisoma hutuba ya ufunguzi kwa
mgeni rasmi, Mwenyekiti wa sasa wa umoja huo ambaye pia ni Mkuu wa idara ya
Rasilimali watu na utawala Bi. Joyce Bakari Mpunga amesema wazo la kuunda umoja
huo lilikuwa ni kuwawezesha wanawake wa Jumuiya ya NIT kujitengenezea kipato
cha ziada nje ya mishahara kwa kupatiwa mafunzo yatakayowasaidia
kujishughulisha na ujasiliamali.
Ametaja malengo mengine kuwa ni kuboresha
mahusiano mazuri mahala pa kazi; kusaidiana katika masuala ya kijamii katika
shida na raha pamoja na kuelimisha na kuhamasisha mazingira bora ya ufanyaji
kazi kwa nidhamu na uwajibikaji kazini.
Aidha akizungumzia idadi ya wanachama wa
umoja huo, Bi Mpunga amesema kwa sasa Umoja huo unawanachama 96 ambao kama
umoja huo utasimama basi itasaidia sana kuboresha hali za akina mama chuoni
hapo na hivyo kufanya Chuo kupata mafanikio mengi kwani bila shaka watafanya kazi
kwa ufanisi wa hali ya juu.
Hiyo
ni Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chuo cha Taifa cha usafirishaji,
Wanawake kuanzisha Jumuiya yenye madhumuni ya kusaidina katika raha na shida. Fullhabari
ilikuwepo katika
eneo la tukio na kujionea mafunzo mbalimbali yakitolewa yakiwemo ya
ujasiliamali pamoja na ya kubadili fikra/matzo yaliyotolewa na YEMCO.
No comments:
Post a Comment