Saturday, March 11, 2017

SERIKALI IZUIE UINGIZWAJI WA NYANYA NA PILIPILI KUTOKA NJE ILI KULINDA VIWANDA VYA NDANI

 SERIKALI imetakiwa kuzuia uingizaji wa bidhaa za Nyanya za kutengeneza pamoja na Pilipili za kutengeneza ili kuweza kuviokoa viwanda vya ndani ambazo zinatengeneza bidhaa hizo.

Pia,Serikali imeombwa kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya masoko pamoja na miundombinu ambayo itasaidia viwanda hivyo kuinuka na kuweza kuzalisha bidhaa nyingi.

Ombi hili kwa serikali limetolewa leo Jijini Dar es Salaam,na Dominicus Ulikaye ambaye ni Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya kiwanda Darsh  ambao ni wazalishaji wa bidhaa za RedGold wakati wa mkutano wa waadau wa Kilimo.

Amesema ili serikali ya viwanda iweze kufanikiwa hakuna budi serikali kuangalia na ikiwezekana kuzuia uingizaji wa bidhaa kutoka nje ili kuweza kuinua bidhaa za ndani.


“Yaani sisi tunazilisha (Tomatos na Chill sause) kwa wingi ila tukakosa masoko ya uhakika kutokana na kupata ushindani kutokana na bidhaa kama hizi ambazo zinatoka nje.ambazo zinapelekea bidhaa zetu kushindwa kutanuka”amesema Ulikaye.

Ulikaye amesema sasa ni wakati wa serikali kutilia mkazo bidhaa hizo kutoka nje kwa kuweza kuziachia bidhaa za ndani kuweza kuuzika vizuri na kusaidia viwanda hivyo ambavyo amedai zimetoa ajira nyingi kwa watanzania.

‘Kiwanda hiki leo kimetoa ajira zaidi ya elfu sitini za wakulima wa nyanya ambao tumekuwa tukizinunua nyanya hizo kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zetu,kwahiyo kwa serikali ikishindwa kuzuia uingizaji wa bidhaa basi watanzania hawa ambao ni wakulima watakosa masoko yetu”ameelekeza Ulikaye.

No comments: