Kituo kipya cha kusaidia vijana walioathirika na madawa ya
kulevya kinachofahamika kwa jina la Mamaz and Papaz Abilitation
Center au maarufu kama
(SOBA HOUSE) chenye makao makuu yake jijini dare es salaam. Na tawi lingine
likiwa singida kinapenda kuwafahamisha watanzania kuwa kimeanza kazi hivi
karibuni na kina takribani mwezi mmoja na kina jumla ya vijana 7. kituo hicho
kinapenda kuwakaribisha vijana wote waliathirika na na dawa za kulevya. Kwani
kituo kina wataalamu mbalimbali wakuweza kuwasaidia ikiwa walimu wakutosha na
madaktari wakiwa tayari kuwahudumia waathirika wa dawa hizo.
EMMI ALLY GHAHAE MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMAZ & PAPAZ AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI JANA JIJIN DAR ES SALAAM |
Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa kituo hicho
Bi. Emmi Ally Gahae alisema yeye ameguswa kwa namna moja au nyingine na tatizo hilo na kuamua kufungua kituo hiko kwa kuwa mwanae ni
miongoni mwa waathirika wa tatizo hilo .
na anapenda kuwahasa wazazi kuleta watoto wao ambao pia ni waathirika ili
waweze kushirikiana nao kwa kuweza kuwafanya wakaacha kabisa na dawa za kulevya.
Na kufanya shughuli nyingine za kijamii.aliongezea kwa kusema Soba House
nyingine ambazo zinawahifadhi baadae wanarudia tena kutumia dawa hizo . lakini
hii ni tofauti kabisa na hizo nyingine kwa kuwa huku wanakaa kwa muda wa miezi
sita na wakimaliza wanapelekwa kwenye work shop. kuwapa furasa ya kuweza
kufanya vitu wanvyoweza kufanya kwani wanawataalamu mbalimbali katika fani
tofauti tofauti kwa ajili ya kuwasaidia vijana hao. kuweza kuachana na matumizi
ya dawa za kulevya na shughuli zenyewe ni kama
kilimo, ufundi mwashi,selemala na umeme kutumia kompyuta na fani nyingi walizo
nazo.
PATRICK CHOKALA BALOZ MSTAAFU (MSHAURI WA TAASISI YA MAMAZ & PAPAZ) |
Na kutokana na taasisi hiyo bado changa inauwezo wa kuchukua
vijana 40 na laengo ikiwa ni kuchukua watu wengi zaidi hata 100 kulingana na
uwezo walio nao. Hivyo basi wanaiomba selikali makampuni na watu binafsi kuweza
kuisaidia taasisi hiyo ili iweze kufika mbali zaidi. Na Iweze kuchukua watu
wengi zaidi ya hao na pia kukidhi kwa mahitaji muhimu kama
chakula mavazi na malazi. Kwani vita ya dawa za kulevya sio vita ya mtu mmoja
tua au ni ya selikali peke yake bali ni ya jamii nzima. Na kwa hili taasisi
hiyo kupitia walimu wake itaweza kupitia
shule mbalimbali nchi nzima lengo likiwa ni kuwafundisha wanafuzi ngazi ya
msingi mpaka sekondari kuweza kupingana na dawa za kulevya kwani zinharibu
nguvu kazi ya taifa.
BW. OMARY RAJABU KOMBE MJUMBE WA TAASISI |
Na tarehe 26 ya mwezi 6 tunajua ni kilele cha kupambana na
dawa za kulevya duniani kote hivyo basi
taasisi hii itafanya tamasha kubwa linao
ambatana na uziduzi wa taasisi hiyo.tamasha hilo litafanyika mkoani
singida na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa mambo ya ndani na taasisi inatarajia
kuwahalika wakurugenzi toka mashirika mbalimbali, mabarozi, viongozi wa
selikali na wadau mbalimbali. Pia mchango wako wa hali na mali
unahitajika katika kufanikisha hilijambo. Pia wanahalikwa vijana wazee kwa
watoto toka maeneo ya karibu kama Dodoma
na sehemu nyingi kuja kwa wingi ili kuweza kupata elimu hii. Taasisi hii
inapenda kuwashukuru wote waliofanikisha kuweza kusonga mbele kwa harakati hizi
na waomba kuungana na selikali katika juhudi hizi.
(Na muandishi wetu Vicent Macha dar es salaam).
1 comment:
Thanks for letting us know the presence of this center i hope it will help to reduce the cases of drugs abuse especially to youths. Together we can help them.
Post a Comment