Rais John Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi wanane waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha Aprili 13 katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.
Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabaraya Dar es Salaam – Lindi.
Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu, familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo.
“Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa, naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu
shupavu.
“Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema RaisMagufuli.
Aidha, Rais Magufuli amelaani tukio hilo na matukio yote ya kuwashambulia askari polisi ambao wanafanyakazi kubwa na muhimu ya kulinda raia na mali na ametaka Watanzania wote watoe ushirikiano katika kukomesha vitendohi vyo.
Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.
No comments:
Post a Comment