Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel imetoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizokuwa zikihihusha kampuni hiyo ya kuisababishia serikali hasara ya shilingi milioni 459 ambapo wao wamehusishwa na vipengele viwili vya mashtaka.
Mashtaka hayo ya Halotel ni kushindwa kutoa taarifa ya usajili wa kampuni ya mitambo ya UNEX Limited ambayo haikuwa kampuni iliyosajiliwa kikamilifu na TCRA kwaajili ya kusajili line za simu 1000 zilizouzwa kwa kampuni hiyo pamoja na kushindwa kutimiza majukumu yao vizuri ya kuuza line za simu 1000.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya mtandao wa simu wa halotel Tanzania Bw. Le Van Dai akitoa ufafanuzi juu ya kesi iliyokuwa ikawakabili kama shirika. |
Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Bw. Le Van Dai amefafanua juu ya kutokuhusika na makosa ambayo yaliwahusisha watuhumiwa wengine ambao ni wateja wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na usimikwaji wa mitambo hiyo.
Alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiendesha ikiendesha shughuli zake nchini kwa kufata sheria na taratibu zote za mawasiliano ambazo zinatambuliwa na mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA).
Bw lai aliongeza kuwa kwa mujibu wa mashtaka yaliyosainiwa na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali kuwa Mei 16 mwaka huu ambayo yanayoitaja kampuni hiyo kuhusika na makosa hayo.
Mwanasheria wa kampuni ya Halotel Bw Christopher Masai akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam. |
Mwanasheria wa kampuni ya Halotel TZ Bi Fatma Seif akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam |
Alisema mujibu kifungu namba 6 na 7 ambavyo havihusishi kampuni hiyo na makosa ya washtakiwa wengine ambao sio wafanyakazi wa kampuni hiyo na kuongeza kuwa hawana ushirikiano wowote na kampuni hiyo pamoja na raia hao wa Pakistani zaidi ya kuiuzia laini za simu kampuni hiyo baada ya kuwasilisha nyaraka zisizo halali.
“Sisi kama kampuni tunafanya kazi kwa usajili na vibali halali vya mamlaka husika nchini na tumekuwa wawazi na kufata vibali kutoka mamlaka husika pamoja na kufata taratibu zote za kisheria " alisisitiza Dai
Waandishi wa habari wakiwa makini kufuatilia ufafanuzi unaotolewa na viongozi wa kampuni ya halotel TZ mapema leo jijini Dar es salaam |
No comments:
Post a Comment