Mzee Philemon Ndesamburo Kiwelu, Mbunge mtaafu wa Moshi mjini amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya KCMC alikokimbizwa kwa matibabu baada ya kujisikia vibaya akiwa nyumbani kwake Moshi.
Jana alimpigia simu Mayor wa Arusha Kalisti Lazaro kwamba aende Moshi akampatie mchango wa rambirambi kwa wanafunzi wa Lucky Vincent. Leo asubuhi Mayor Kalist na kamanda Bahati David wakasafiri kwenda Moshi kupokea mchango huo. Wakati mzee Ndesamburo anaandika cheque akaishiwa nguvu. Wakamkimbiza KCMC ambapo mauti imemfika huko.
Nimepokea kwa mshtuko taarifa za kifo cha Baba yetu huyu. Mwanzoni mwa mwezi huu tulimtembelea nyumbani kwake, mimi na Kamanda Imma Saro. Tulimpigia simu kumsalimia akatualika nyumbani kwake. Tukasafiri kutoka Arusha tukaenda kumuona Moshi. Alikua na afya njema. Tulizungumza mengi, akitushauri na kutufundisha mambo mbalimbali kuhusu siasa. Sasa ndio nagundua kwamba aliikua akitupa wosia.
Pumzika kwa amani baba. Umepigana vita njema, kazi umeimaliza. Tutaonana Paradiso.!
Malisa GJ
No comments:
Post a Comment