Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekemea vikali vitendo vya mauaji
vinavyoendelea sehemu mbalimbali kote nchini .
Akiongea na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi mkuu Bi. Anna Henga alisema kuwa vitendo vinavyoendelea kwa sasa vya
mauaji ya polisi pamoja na Raia ni ukiukwaji wa haki za binadamu na vinatakiwa
kukemewa haraka iwezekanavyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu Bi. Anna Henga akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam |
Tumeweza kuona matukio yaliyotokea sehemu mbalimbali ikiwa
Tanga, Geita pamoja na yanayoendelea huko kibiti mkoani pwani yanayohusisha
mauaji ya viongozi wa vijiji ikiwa kijiji cha nyabuda, mkandawala, kaza moyo na mwenyekiti wa ccm
makondeko pamoja na mkuu wa kituo cha polisi.
Hali hii inawafanya wananchi wa maeneo hayo kuweza kuishi
kwa woga kutokana na vitisho vya askari wenye bunduki wakipita pita maeneo yao
ya kazi. Hali hii inadhorotesha uchumi wanchi kutokana na raia kushindwa
kufanya shughuli zao kwa uhuru kuhofia kukamatwa na waliowengi kushindwa kwenda
hata mashambani na wengine kazi zao zinaanza kuchanganya kuanzia usiku kama
chipsi lakini wanashangazwa na serikali kutoa onyo kuwa kwa maeneo hayo kwepo
mwisho saa 12 jioni.
Mkurugenzi wa ufuatiliaji ukiukwaji wa haki za binadamu na uwajibikaji (DHA) Felista Mauya akitilia mkazo alichokiongea kaimu mkurugenzi mtendaji |
Kituo cha sharia na haki za binadamu kimetoa mapendekezo
ikiwemo kurudishwa kwa polosi jamii kwa kuweza kubaini watendaji wa haya ni
nani?.
Askari kuweza kuboreshewa mafunzo yanayoendana na wakati
uliopo wa sayansi na teknolojia na sio kutumia nguvu kwani wanowaumiza ni raia
na siyo waalifu kama wanavyodhani.
Kupelekwa watafiti waweze kuchunguza kuwa wanofanya mambo
haya wanatoka wapi na sio kukurupuka na kuanza kuonea raia kana kwamba wao ndio
wanotekeleza mauaji hayo.
Na wananchi hususani vijana kupewa elimu ya uraia ili waweze
kuwa na uzaredo na nchi yao na kuacha
kujichukulia sharia mikononi.
No comments:
Post a Comment