Thursday, May 18, 2017

Kwa mara ya kwanza Manara amewapongeza Yanga


Waswahili wanamsemo wao usemao ‘asiyekubali kushindwa si mshindani’ kauli hii inathibitishwa na Haji Manara msemaji wa Simba anaetumikia kifungo cha mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka.

Mara baada ya ushindi wa Yanga wa goli 1-0 dhidi ya Toto Africans na kuusogelea ubingwa wa VPL kwa asilimia 99, Manara amewapongeza Yanga kwa hatua waliyofikia.
Kupitia ukurasa wake wa instagram @hajismanara ameandika ujumbe unaosomeka: “Uungwana wa mpira tumezaliwa nao, hongereni watani, mapambano bado yanaendelea.”
Kupitia ujumbe huo, Manara ameonesha 'fair play' na weledi wa hali ya juu kwa kuonesha heshima kwa Yanga na kutambua fika nguvu waliyoitumia Yanga kuvuna walichokipanda.

No comments: