Monday, May 22, 2017

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA) KUFANYA UKARABATI WA MIUNDO MBINU YA SHULE YA SEKONDARI MZUMBE NA KILAKALA - MOROGORO

Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Graceana Shirima (katikati) akimuelezea mwandishi wa habari wa ITV, Bw. Sifuni Mshana (kulia) kiasi cha fedha itakayotumika katika ujenzi wa awali wa miundombinu ya shule mbili kongwe za kilakala na Mzumbe mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua kiwango cha uchakavu wa miundo mbinu hiyo.
Mshauri muelekezi wa Nousoto Associates, Bw. Thomas Kalugula akitoa taarifa ya upembuzi yakinifu wa mahitaji ya ukarabati wa shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro na kubainisha kuwa, ujenzi wa awali utahusisha mifumo ya maji taka ambayo haifanyi kazi ipasavyo huku akihaidi kuwa watasimamia ujenzi huo hadi hatua ya mwisho.
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Morogoro, Bi. Veneranda Seif akikabidhiwa mkataba wa ujenzi wa shule kongwe za Kilakala na Mzumbe ambazo zilielezwa kugharimu kiasi cha shillingi billioni mbili katika ujenzi wa awali huku mkataba huo ukimtaka mkandarasi huyo kuanza ujenzi mapema 2 Juni mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu (TEA), Bi. Graceana Shirima akiwa na timu ya wataalamu wakiwemo waandishi wa habari mkoani Morogoro katika kukagua miundo mbinu ya shule ya sekondari Kilakala ili kujionea hali halisi ya majengo na kubaini uwepo wa jengo ambalo halitumiki kutokana na kukosa ukarabati.
Walimu wa shule ya Mzumbe mkoani Morogoro na wakandarasi wakiwa na kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Graceana Shirima wakiangalia shimo la maji taka ambalo lilielezwa kuwa limetitia likazuiwa na magogo kwa tahadhari zaidi hata hivyo majani yanaoneka yameota katika eneo hilo huku likisikika kutoa harufu kali ya vinyesi.
Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Gracean Shirima (katikati) akiwa darasani kukagua dali zilizotoboka katika moja ya jengo la kujifunzia shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro.
Timu ya watalaamu wakiwa na mkandarasi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoa wa Morogoro, Bi. Veneranda Seif (wa pili kutoka nyuma) katika ziara ya Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Gracean Shirima akikagua majengo yaliyochakaa.
Bweni la wanafunzi kama linavyoonekana.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mzumbe, Mwalimu Wencelaus Kihongoti akimpa maelekezo machache Afisa uhusiano wa TEA Silvia Lupembe.
Afisa uhusiano wa TEA Silvia Lupembe akibadilishana mawazo na wafanyakazi wenzake.
----
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetenga kiasi cha shilingi billioni mbili ili kukarabati miundombinu ya shule kongwe za Sekondari za kilakala na Mzumbe kwa wamu ya kwanza ikiwa ni kuboresha kiwango cha elimu na kurudisha umaarufu wa shule hizo ambazo zimetoa wasomi wakubwa na watalaamu mbalimbali hapa nchini.
Akiongea katika makabidhiano ya mikataba ya ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu ya shule kongwe ya Mzumbe sekondari na kilakala sekondari mkoani morogoro Kaimu mkurugenzi mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Gracean Shirima amesema ukarabati wa shule hizo umeingia mkataba na mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa gharama ya shillingi Billioni 2 kwa awamu ya kwanza huku meneja waShirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bi. Veneranda Seif amehaidi kuhakikisha ujenzi wa miundo mbinu hiyo unafanyika kwa kiwango kikubwa kuhakikisha thamani ya fedha iliyotolewa inatumika kikamilifu.
Kwa upande wake mshauri wa mradi, Bw. Thomas Kalugula amesema katika upembuzi yakinifu kuna sehemu ya miundo mbinu inatakiwa kufanyiwa ukarabati ikiwemo mifumo ya maji taka katika shule hizo huku wanafunzi wakiipongeza mamlaka ya elimu Tanzania kwa kuwandalia mazingira bora ya kujisomea.

No comments: