Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, jana alioongoza
mashekhe ikiwa ni utamaduni wa kukaribisha mfungo wa mwezi mtukufu wa
ramadhani.
Dua hiyo iliyofanyika Tambaza makaburini, Upanga Mashariki Jioni , iliaambatana na dua za kuwaombea marehemu wote ambao walikuwa vipenzi vya mtume na watumishi wa Quruan hususani aliyekuwa mtabiri wa Nyota hapa nchini, Shekhe Yahya Hussein aliyetangulia mbele ya haki.
Dua hiyo iliyofanyika Tambaza makaburini, Upanga Mashariki Jioni , iliaambatana na dua za kuwaombea marehemu wote ambao walikuwa vipenzi vya mtume na watumishi wa Quruan hususani aliyekuwa mtabiri wa Nyota hapa nchini, Shekhe Yahya Hussein aliyetangulia mbele ya haki.
kipenzi cha Mtume Muhamad (S.a.W), ambaye pia ni mjukuu wa marehemu Shekhe Yahya Hussein, Yahya Hussein wakati akisoma Quruan Tukufu katika Makaburi ya Tambaza Jijini Dar es salaam jana
|
Katika Dua hiyo, tulishuhudia baadhi ya vipenzi vya mtume,
wakisoma Quruan Tukufu pamoja na
mashairi mbali mbali, miongoni mwa vipenzi vya mtume ambao walisoma Quruan ni
pamoja na Hassan Nassoro Amrani, Hussein Nassoro, Mohamed Nassoro Amrani,
halikadharika na Yahya Hussein ambaye ni mjukuu wa marehemu Shekhe Yahya
Hussein.
Aidha akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa
Shekhe Yahya Hussein Foundation,Mohamed Nassoro Amrani, alisema kuwa , lengo la
dua lilikuwa ni kuwaombea marehemu wote waliojitoa kwa maslahi ya dini ya
kislamu pamoja na watumishi wa Quruan Tukufu akiwemo Shekhe Yahya Hussein.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa, pamoja na dua hiyo lengo
walilenga kuwa na dua ya pamoja kwa ajili ya kuukaribisha mfungo wa mwezi mtufu
wa ramadhani unaotarajia kuanza hivi karibuni ambapo waisalamu wote watatkiwa
kufunga mwezi huu ili kuweza kukamilisha nguzo ya kislamu katika nguzo tano
walizo nazo.
.Meya Isaya Mwita, akipokea dua jana wakati wa kisomo cha kuwaombea marehemu na kukaribisha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani katika viwanja vya Tambaza Makaburini Jijini Dar es salaam jana
|
“Tumekuwa ni utaratibu wetu wa sisi waislamu pamoja na
Foundation ya kufanya dua kila mwaka kwa ajili ya kumkumbuka mtumishi wa Quruan
Tukufu marhemu Shekhe Yahya,mbali na kumkumbuka ni utamaduni wetu kila ikariapo
mfungo wa mwezi wa ramadhani tunakuwa na dua maalumu ya kuukaribisha na
kukumbusha mazuri ambaayo tunatakiwa kufanya na kuyakataza yale mabaya ambayo
yalipingwa katika kipindi hiki ili kuendeleza dhima nzima ya Uislamu na
mazingatio yake kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha Quruan”, alisema Amrani
Pia akisoma risala fupi mbele ya mgeni rasmi, Yusuph Momba,
alisema anawapongeza Pepsi kwa mchngo wao wa kutoa mahema pamoja na kujenga
ukuta kwani eneo hilo lilikuwa ni eneo la maovu kama vile uvutaji bangi, vibaka
na vitendo vingine visivyo na usalama kwa jamii, lakini mbali na msaada huo bado wana deni kwa
mkandarasi hivyo wamemuomba Mstahiki Meya aliangalie swala hili kwa kina na
kuweza kuwasaidia kulipa deni hilo
Akizungumza na waandishi wa habari, Meya wa Jiji la Dar es
salaam, Isaya Mwita, aliwataka waislamu kuendeleza mema aliyoyaacha mtume
Muhamad (sw) huku na kilinda heshima ya watumishi waliotangulia katika
kuhakikisha umma wao unakuwa salama na kuimarisha mshikamano wao katika kuelekea mfungo wa mwezi
mtukufu wa ramadhani unaotarajia kuanza mwiahoni mwa wiki hii ili kutimiza nguzo tano za uislamu.
“Changamoto nimezisikia naombeni mnitajie deni lililopo
naweza kulilipa lote au kulipunguza pia wale walichonacho pia wajitahidi kutoa
kwa ajili ya kujenga umma wao waache ubahili wakiwa bahaili hata matumizi yao
mungu hata yanyoosha kwa njia slama watajikuta wakifanya vitu vizuri ambavyo
havidumu hivyo nawaaombeni katika kuelekea mwezi huu tuanye mema “,alisema Meya
Mwita
No comments:
Post a Comment