Mmoja wa washiriki wa michuano ya ngumi ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, akipima uzito kuashiria utayari wa ushiriki wa pambano hilo ambapo jumla ya timu 14 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam kesho jioni
Mjumbe wa kamati ya maendeleo ya Vijana ya ngumi na mkufunzi wa DABA, Juma Uweso, akizungumza na mwandishi wa habari kuhusu maandalizi katika kuelekea kwenye michuano ya pambano la Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita, yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho jioni kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa chama cha mchezo wa ngumu Mkoa wa Dar es salaam, Wamboi Mangole, akizungumza na waandishi wa habari , hawapo pichani wakati wa zoezi la upimaji wa uzito wa washiriki wa mchezo huo .pambano hilo limeandaliwa na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita. linatarajiwa kupigwa kesho jioni kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam .
Mkufunzi wa chama cha ngumu mkoa wa Dar es salaam, Mohamed Bamtula, akiendeleaa na zoezi la ujazaji fomu za washiriki wa michuano ya ngumi ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Magereza wakiwa na kocha mkuu wa timu hiyo , Antony Kameda (mwenye koti la kijani) wakati wa zoezi la upimaji uzito katika kueleka kwenye michuano ya Meya cup mkoa wa Dar es salaam leo.
Timu ya Magereza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upimaji uzito wa michuano ya ngumi mkoa wa Dar es salaam inayodhaminiwa na Mstahiki Meya wa jiji Isaya Mwita.
Mwana dada kutoka JKT akiwa katika upimaji uzito wa mashindano ya ngumi mkoa wa Dar es salaam leo , huku akionekana ni mtu mwenye kujiamini licha ya mchezo huo kutokuwa na washiriki wengi upande wa wanawake.
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MABONDIA wa mashindano ya ngumi ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo wamepimwa uzito tayari kwa mpambano huo hapo kesho.
Washiriki wa mpambano huo kutoka jiji la Mombasa, sambamba na mabondia waliopo katika Halmashauri ya jijini hapa walifika kufanyiwa vipimo hivyo mapema asubuhi ya leo ambapo jumla ya washiriki 72 walifanyiwa vipimo hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo, Mratibu wa mashindano hayo, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha ngumi mkoa wa Dar es Salaam Wamboi Mangole amesema kuwa baada ya hatua hiyo ya awali ya kupima uzito, kesho wataingia kwenye mpambano huo utakao anza saa 10:00 jioni.
Alifafanua kuwa mashindano hayo ni ya nne tangu kuanzishwa ambapo kwa mwaka huu, yamedhaminiwa na Mstahiki Meya wa Jiji Mwita nakusema kuwa yamekuwa ni mashindano yenye msisimko mkubwa zaidi.
" Kama mnavyoona leo ndio tupo kwenye hatua ya upimaji wa uzito, baada ya kumaliza tutafanya kazi ya kupanga nani atashindana na yupi kwenye mpambano huo hapo kesho" amesema Mratibu.
Aidha alifafanua kwamba , katika mashindano hayo walialika timu mbalimbali kutoka nje ya Nchi ambapo hadi zoezi la upimaji uzito alinafanyika , mabondia sambamba na kocha kutoka Mombasa Kesha walikuwepo kwenye mchakato huo.
Timu nyingine zilizo ripoti kushiriki mpambano huo na kupimwa uzito ni Jeshi la Wananchi (NGOME), Jeshi la kujenga Taifa (JKT), Polisi Magereza, Timu za jiji la Dar es Salaam pamoja na mzizima.
Mpambano huo unatarajiwa kufunguliwa na Mstahiki Meya wa jiji Mwita kesho saa 10:00 ambaye ndiye mdhamini mkuu wa mashindano hayo.
Kwaupande wake Katibu Mkuu wa Chama cha ngumi jijini Mombasa ,Chrispine Onyango amesema kuwa ujio wao ni kwa ajili ya kuchukua kombe hilo la Mstahiki Meya wa jiji licha ya changamoto walizokuwa nazo.
Amefafanua kuwa awali walitakiwa kuja timu ya watu saba kwa ajili ya ushiriki wa mpambano huo,lakini kutokana na sababu za kisiasa nchini huo, kukosa wadhamini wamelazimika kuja na mshiriki mmoja aliyemtaja kwa jina la Mohamed Ally mwenye uzito wa Kg.49.
Katika mpambano huo ambao utaanzia na Kg 49, mshindi wa kwanza atajinyakulia kombe , wakati mshindi wa kila uzito watapatiwa zawadi za medali ikiwemo Dhahabu, Shaba, pamoja na Silva.
Naye mjumbe wa kamati ya maendeleo ya vijana na mkufunzi wa Chama cha ngumi mkoa wa Dar es Salaam (DABA) Juma Uweso alimpongeza Meya wa Jiji kutokana na kujitolea kudhamini mashindano hayo na kutumia nafasi hiyo kuomba wadau wengine kujitokeza.
No comments:
Post a Comment