Sunday, May 28, 2017

NAODHA WA SIMBA APATA AJALI MBAYA SANA.

Siku moja baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya Simba dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Jamhuri Dodoma na Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2-1, leo May 28 nahodha wa timu hiyo Jonas Mkude ameripotiwa kupata ajali.
Jonas Mkude
Mkude ambaye alikuwa katika gari binafsi na baadhi ya watu amepata ajali ya gari akitokea Dodoma akiwa maeneo ya Dumila mkoani Morogoro akiwahi Dar es Salaam kwa ajili ya kambi ya timu ya taifa Taifa Stars.

Gari waliyopata nayo ajali Jonas Mkude na abiria wengine
Taarifa za awali zinasema mkude kaumia maeneo ya shingo na mmoja kati ya waliokuwemo ndani ya gari hilo amefariki dunia.

No comments: