Wednesday, May 24, 2017

TIB CORPORATE BANK YATIMIZA AGIZO LA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUFANYA KAZI MASAA 24 KWA TAWI LAKE DOGO LA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Akitoa ta taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Benki hiyo Bw.Frank Nyabundege amesema wameamua kutoa huduma hizo ikiwa ni sambamba na kuitikia agizo la Mh.Rais wa Jamuhuri ya mungano wa Tanzania alipozitaka taasisi zote husika katika bandari kutoa huduma siku zote kwa masaa 24.

"Benki ya TIB Corporate tayari imeanza kutoa huduma za kibenki kwa siku zote kwa masaa 24 katika tawi dogo la TPA lililopo ndani ya eneo la bandari."alisema
Mkurugenzi wa TIB corporate Bw Frank Nyabundege akitoa ufafanuzi kuhusu benki yake kufanya kazi kwa masaa 24, na kushoto ni Meneja masoko wa benki hiyo Bi. Theresia Soka


Bw.Nyabundege ameeleza kuwa benki yake imejipanga vyema ili kuhakikisha huduma hii inaleta ufanisi na urahisi zaidi kwa mlipaji kwani wataweza kulipa kodi za aina mbali mbali na tozo zote za bandari kupitia tawi hilo dogo ili ziweze kutumika katika kuleta maendeleo ya nchi kupitia mapato hayo.

 Aidha,benki hii yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya akaunti za mamlaka ya bandari -TPA,imekwisha ingia mkataba na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuunganisha mfumo wa malipo ya kodi ujulikanao kama TAXBANK hivyo mlipa kodi akilipa katika tawi lolote la benki taarifa zake zitaonekana mara moja katika mtandao wa TRA kwa haraka na ufanisi zaidi huku mlipaji akiendelea na taratibu zingine.

Hata hivyo,TIB Corporate bank ni benki ya kibiashara inayomilikiwa na serikali kwa 100% lakini inatoa huduma za kibenki na biashara kwa taasisi na mashirika ya serikali na binafsi huku ikiwa na matawi sita ikiwemo Dar es salaam matatu(3),mwanza,arusha na mbeya ikiwa na tawi moja kila mkoa.

Baadhi ya viongozi wa TIB corporate benki kushoto ni Mkurugenzi wa biashara Mwalu Mwachang'a, kati ni mkurugenzi wa mikopo Adolphina William, na kulia Mkurugenzi wa kazi ni Karoli Shayo wakifuatilia mkutano
Pia aliongeza kwa kusema kuwa wameshaanza mchakato wa kuweka matawi kwenye kila bandari na wanaanza na Tanga pamoja na Mtwara na baadae kuweka nchi jirani kama congo na nyinginezo.

Bw. Bundege alipenda kuwaomba waandishi wa habari kuweza kujulisha wananchi wote wajue kuwa TIB corporate benki wapo bandarini kwa masaa 24 hivyo hata mizigo yao itaingia usiku na wanaweza kulipa kodi na kutoa kwa muda husika.

Jopo la viongozi wa TIB corporate benki wakiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam

Waandishi wa habari wakichukua matukio kwenye mkutano wa benki ya TIB corporate na wanahabari uliofanyika makao makuu ya benki hiyo Samora jijini Dar es salaam

No comments: