Thursday, June 15, 2017

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya kinondoni mapema leo limekutana kwa ajili ya kujadili bajeti ya halmashuri hiyo ya mwaka 2017/2018 . lakini pia kumpongeza rais magufuli kwa kazi kubwa anyoifanya katika serikali ya awamu ya tano. Baraza hilo lililokutanisha madiwani toka kata mbalimbali za wilaya ya kinondoni pamoja na kujadili utendaji kazi na mipango ya halmashauri hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashuri ya Kinondoni Mh. Beni Samweli Sita akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam

Akiongoza kikao hicho kilichodumu kwa takribani saa moja na nusu Mstahiki Meya wa wilaya Kindondoni Mh. Beni Samwel Sita aliwaomba madiwani kuwa watulivu na wasikivu ili agenda ziwekwe mezani na zoezi la kuzijadili lianze mara moja ili kuweza kupata muhafaka.

Pia Mh. Ben Samwel Sita pamoja na Madiwani walichukua wasaa huo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Joseph Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kulinda rasilimali za nchi na pia kuwawajibisha viongozi wasio waaminifu kwenye serikali yake. Lakini pia kwa kuweza kugundua wizi uliokuwa kwenye mchanga (makinikia) ya dhahabu na madini mengineyo. Na kuweza kuwawajibisha viongozi waliotumia vibaya madaraka yao kuweza kutaifisha rasilimali za Watanzania.


Lakini pia kitu kingine baraza hilo liliweza kujadili kuhusu kupewa mamlaka ya utekelezaji kwa serikali za mitaa na kata ili kuepuka tatizo  kucheleweshwa kwa miradi ndani ya kata. Na utekelezaji si mpaka kusubiri ngazi ya juu ambayo ni halmashauri kuja kusimamia fedha zinapotolewa zoezi liweze kuanza mara moja.

Diwani wa kata ya Mwananyamara ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Muindo Mbinu Bw. Songoro Mnyonge akiwasilisha ripoti ya kamati yake ya miundo mbinu mapema leo jijini Dar es salaam


Diwani viti Maalum kata ya Mikocheni Bi. Matha Chares Mtiko akichangia hoja kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ambaye pia ni Diwani Viti Maalum wa Kata ya Kinondoni Bi.Tatu Maliaga akiwasilisha ripoti yake ya maadili katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya  Kinondoni

Diwani viti Maalum kata ya Bunju Bi. Caroline Faustine Kazinza akitoa mapendekezo kwenye mkutano wa Baraza la madiwani uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam

Diwani wa Makongo Ndeshukuru Ntangaraza akichangia mada kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani Wilaya ya Kinondoni uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam 

Baadhi ya madiwani wa Kata mbalimbali za Halamshauri ya Wilaya ya Kinondoni wakifuatilia kwa ukaribu kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam


No comments: