Wazazi kote nchini wametakiwa kuwaharakisha matibabu watoto
wao endapo watagundua kuwa wana matatizo ya kichwa kikubwa au mgongo wazi. Hayo
yameelezwa leo Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji
Taasisi ya Tiba na Mifupa ya MOI Dr. Respicious Boniface alipokuwa akipokea
misaada ya dawa toka Diamond Trust Bank wakishirikiana na E Fm Radio.
Mkurugenzi Mtendaji wa Diamond Trust Bank Tawi la Morroco Bi. Sheena Y. Sinare akitembelea hodi za Watoto wenye Vichwa vikubwa na migongo wazi kwenye Taasisi ya MOI Muhimbili jijini Dar es salaam |
Akiongea na waandishi wa Habari Dr. Respecious Boniface alipenda
kuwashukuru DTB na E FM na alipenda kuwaomba wazazi wamuwaishe mapema pindi
wanapogundua kuwa mtoto anatatizo moja wapo kati ya hayo kwani ukiwahi mtoto anapona
na hata matibabu yake yanakuwa hayana
usumbufu sana kama unapomchelewesha.
Pia aliongezea kwa kusema tatizo hili sio Tanzania peke yake
bali ni dunia nzima na tathmini inaonyesha kila kwenye watoto 1000 wanaozaliwa Duniani
wawili lazima watakuwa na tatizo hilo. Na miongoni mwao asilimia 70 ni wenye Vichwa
vikubwa na asilimia zilizobaki 30 ni wa Mgongo wazi.
Mkurugenzi wa DTB Tawi la Morroco Sheena Y. Sinare akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dr. Respicious Boniface misaada ya Dawa iliyotolewa mapema leo Muhimbili jijini Dar es salaam |
Na Dr. Respecious Boniface alipenda kuzishauri Taasisi
mbalimbali, Idara za Serikali na watu binafsi kuweza kuiga mfano wa DTB na E fm
kwa kuwa na utaratibu wa kujitolea misaada kwa magonjwa mbalimbali ambao hawana
uwezo. “Na wapo wengi sio tu kitengo cha MOI bali hata magonjwa mengine kama kansa
na magonjwa mengineyo”.Alisema
Lakini pia afsa habari wa Diamond Trust Bank(DTB) Mr.Baguma Ambary alipenda kushuru wauguzi wa MOI kwa mapokezi yao mazuri na kuwaomba waendelee na
moyo wa kujitolea kwa wagonjwa hao kwani sote tunafahamu kazi ngumu waliyonayo.
Na pia alipenda kushauri taasisi mbalimbali kuweza kujitolea kama wao na siyo
kila ifikapo siku ya Mtoto wa Afrika wao kwenda kuwaona Yatima pekee waangalie
na watoto wanaoteseka kwa magonjwa kama hayo.
No comments:
Post a Comment