24th May 2017, Dar es Salaam.
Exim Bank Tanzania imetambuliwa kama Benki bora ya mwaka katika wateja binafsi na biashara
ndogondogo na saizi ya kati,
yaani ‘Retail banking’ katika tuzo za Banker za Afrika Mashariki zilizofanyika
Nairobi, Kenya.
Tuzo za Banker za
Afrika Mashariki zimedhamiria kuhamasisha ubora kwenye sekta ya fedha katika kanda
ya Afrika Mashariki. Kupitia kura 77,000 zilizopigwa na jamii ya sekta ya fedha
katika kanda hii benki ya Exim ilichaguliwa kama mshindi wa mwaka huu katika
wateja binafsi na biashara ndogo - Retail.
Akiongea kwa niaba ya
benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha fedha Selemani Ponda alisema, “Tunajivunia sana
na kushukuru kwa tuzo hii. Tumefanya kazi kubwa kwa muda mrefu kujenga msingi
wa kuendeleza operesheni zetu za baadae. Matokeo yanajionyesha, katika miaka ya
karibuni amana kutoka kwa wateja wetu imeongezeka na wateja pia wameongezeka.
Vilevile faida baada ya kodi imeendelea kukua hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni
72 kwa mwaka 2016.”
Ponda ambaye alihudhuria hafla ya tuzo
hizo alitoa pongezi kwa waandaaji kwa kuandaa tukio lenye mafanikio kwa miaka
mine mfululizo. Hadi sasa tuzo hizo zimevutia ushiriki wa wanataaluma wengi
zaidi katika sekta ya benki katika kanda hii. Zaidi ya hapo aliongeza kuwa
washirika muhimu kama vile kampuni za teknolojia ambazo husaidia kubadilisha
sekta hii pia zilitambuliwa kwa mchango wao.
Mkuu wa kitengo cha
wateja binafsi na biashara ndogo Rahul Singh, alisema kuwa uvumbuzi pia
umechangia kwa kiasi kikubwa katika kuifanya Exim kuwa benki bora nchini
Tanzania na inaheshimika sana katika utoaji huduma na operesheni kupitia jukwaa
la kiwango cha juu katika teknolojia. “Uvumbuzi ni ahadi tunayowapa wateja
wetu. Benki hii imepata upenyo mkubwa kwa kuweka teknolojia ya viwango vya
kimataifa na bidhaa zinazolenga mahitaji ya wateja,” aliongeza.
Benki ya Exim bank imechukua hatua nyingi katika kitengo hiki ikiwa ni pamoja na kuanzisha huduma ya kipekee inayoitwa "Preferred Banking" ambayo inaruhusu mteja kupata mhudumu wa benki wa kumhudumia, huduma za kipekee katika matawi ya benki, bei upendeleo ya bidhaa na faida za kipekee za kimaisha. Benki ya Exim ilikuwa ndiyo ya kwanza nchini kutambulisha kadi za kimataifa za malipo za MasterCard na Visa Platinum, Tanapa na kadi za Visa za malipo baadaye. Benki hii pia ilianzisha matumizi ya mashine za kutolea fedha yaani ATM na mpango wa mikopo kwa wanawake Tanzania.
Juhudi za uanzilishi za Exim zimepitiliza mipaka, mwaka 2007 ilikuwa ni benki ya kwanza kuwa na operesheni nje ya nchi katika nchi ya Comoro. Benki ya Exim pia iliendelea kutanua mbawa zake zaidi katika nchi ya Djibouti Machi 2011, na kuweza kuunganisha kimkakati nchi hizi zilizo katika pembe ya Afrika. Mwaka 2016, Benki ya iliejitanua zaidi kikanda kwa kuwa na matawi matano nchini Uganda.
Singh alimalizia kwa
kuitambua timu nzima ya benki hiyo haswa wanaotoa huduma moja kwa moja kwa
wateja katika matawi ya benki kwa kazi nzuri na kutimiza wajibu wao ipasavyo.
Pia aliwashukuru wateja wote wa benki ambao wamechagua kuwa nao na ambao
wanaisaidia benki hiyo kuweza kupata mafanikio kwa kuwapa biashara. Benki
inajikita kuendeleza mindombinu yake, kuboresha huduma kwa wateja na operesheni
ili kutoa huduma za kiwango cha juu kwa wateja.
No comments:
Post a Comment