Friday, June 9, 2017

ORIFLAME YASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UTOAJI HUDUMA NA UUZAJI BIDHAA ZAKE ZA VIPODOZI DUNIANI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kusheherekea miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Wapili kushoto ni Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina Rangnitt, Mtaalamu wa masuala ya siasa na biashara kutoka ubalozini, Ludvig Bontell na Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu.
 Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina Rangnitt (wapili kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kutimiza miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra,Mtaalamu wa masuala ya siasa na biashara kutoka ubalozini, Ludvig Bontell na Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu. 
 Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kutimiza miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Wapili Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina. 
 Balozi wa bidhaa za Oriflame Tanzania, Missie Popular akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kutambulishwa na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo katika nchi za Afrika Mashariki, Mary Riungu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani.

Baadhi ya wadau waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za Oriflame, wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi wakuu wa Kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VENANCE NESTORY)

No comments: