Thursday, June 1, 2017

TIZAMA PICHA ZA MAZOEZI YA TAIFA STARS JANA USIKU

Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu (kushoto) na Said Ndemla wakiwania mpira katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria leo asubuhi Juni 01, 2017. Taifa Stars inayodhaminiwa Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.

Makipa wa Taifa Stars kutoka kushoto, Said Mohammed, Aishi Manula na Benno Kakolanya wakivuta pumzi baada ya mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. Taifa Stars inayodhaminiwa Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.



No comments: