Ubunifu unaojielekeza kuleta mabadiliko katika bima ndio msingi wa kukua
kwa sekta hiyo kama anavyosema mtaalamu wa masuala ya bima. Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mwandamizi wa taasisi ya
bima ya Resolution Insurance (RI) Mary Anne Mugo katika mahojiano na mwandishi alisema
kuwa moja ya mikakati
mikubwa ya kukuza sekta ya bima ni kupitia kuwa na mkusanyiko anuai wa bidhaa na
wakati huo huo kuwaelimisha wananchi umuhimu na usahihi wa kuwekeza katika kuwa
na bima.
Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni Mugo alibainisha kuwa kutofahamu kwa wananachi umuhimu wa
kukabiliana na majanga ni
moja ya sababu zinazosababisha sekta ya bima kutokua kwa kasi. Alisema kwamba bila kuwekeza katika kuwaelimisha watu kuhusu huduma
zinazotolewa, sekta hiyo haiwezi kutekeleza mchango wake katika kukua kwa
uchumi na maendeleo ya nchi kwa jumla. Alidokeza umma sio tu kwamba ni lazima
utaarifiwe kuhusu bima lakini pia uhamasishwe kuziwekea
bima mali zao pamoja na bima za maisha.
“Kuhamasisha kuhusu soko letu kumekuwa kunaendelea kwa
kusambazia wamachama sio kwa Tanzania tu bali pia nchini Kenya, Uganda Sudan
Kusini ambao ni wananachama
wengine wa Jumuia ya Afrika Mashariki ambako
tunaendesha shughuli zetu,” alisema Mugo.
”Ufahamu kuhusu huduma na sekta pia ni muhimu katika
kukua kwake pamoja na
uchumi wa taifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla,” aliongeza na kubainisha kuwa
sekta hiyo ya kifedha ni muhimu katika
Nyanja yoyote ile ya uchumi.
Mugo alitoa mapendekezo yake akisema, “Watu ni lazima
wafahamishwe mchango
unaotolewa na mabenki, mashirika ya bima, mifuko ya pensheni, masoko ya mitaji,
na hali kadhalika maduka ya fedha kwa
sekta ya fedha ni nyanja muhimu
katika kukua kwa uchumi na maendeleo.”
Resolution Insurance ilianzishwa mwaka 2008 kama
kampuni ya udalali lakini
baadaye ilibadilishwa na
kuwa kampuni ya bima mwkaa 2012 na kwa kasi ilijipenyeza katika soko la bima la ndani na ukanda,
ambapo katika hatua za awali ilikuwa inatoa bima ya afya pekee. Hata hivyo kwa
mujibu wa Mugo, RI hivi sasa ina bidhaa nyingi kwa ujumla zinazohusiana na
bima zikiambatana
na kuwakinga wateja dhidi
ya aina mbalimbali za majanga ambayo
vinginevyo yangesababisha hasara kama wasingekuwa wamejiwekea bima
dhidi ya majanga hayo.
Alibainisha kuwa bima hizo zinahusu magari, afya,
moto, ajali, mali, usafiri, (barabara, majini na angani) na nyingine. “Tumelenga mipango ya thamani ya sera ya bima ambayo
inakubalika kwa mahitaji ya wateja wetu”, alisema Mugo na kuongeza kwamba
kampuni hiyo ya bima hivi sasa inatoa sera
ya biashara ya jumla isiyo
katika madaraja ya tiba ili
kuongeza thamani ya uwiano na nafasi kuifanya kampuni kuwa kituo kimoja cha
huduma zote kwa wateja wake.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, kwa ujumla
bidhaa za bima isiyo ya tiba inajumuisha dhamana ya kuaminiwa, bima ya
wacheza gofu, dhamana, uhalifu, bima ya vifaa vya kompyuta na umeme,
makandarasi, majanga yote, amana za wafanyakazi, hasara inayosababishwa na
moto, bima ya moto, bidhaa inayosafirishwa, kuharibika kwa mashine, bidhaa
zinazosafirishwa kwa njia ya majini, fedha zinazosafirishwa, bima ya kituo cha mafuta (petroli) na bima ya
mitambo (bima zote).
Nyingine ni pamoja na bima ya kuta za vioo, amana za
umma, fidia ya mfanyakazi, bima ya kaya, bima za magari ya biashara na magari
binafsi. “Katika dhana ya kuhakikisha
kuwa wananchi
wanaelewa faida za bima
tunaandaa mazungumzo kuhusu afya, mikutano na kupimwa afya bure, na kwa njia
hii tunawashauri wateja wengi kadri
iwezekanavyo kujiunga na
mipango yetu ya bima”, alisema Mugo.
Takribani asilimia
0.7 ya upungufu katika pato la taifa kunaufanya
upenyezaji wa bima kuwa
mdogo ambapo wadau wa kisekta wanabainisha kuwa kukosekana kwa sera ya taifa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazozuia
kufikiwa kwa bima miongoni mwa wananchi. Hata hivyo Mamlaka ya Usimamizi
wa Bima Tanzania (TIRA) ilikadiria kupenyeza kwa bima kukuwa kungeweza
kufikia silimia 0.9 mwaka 2016.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizopo sekta ya bima Tanzania ina wachangiaji 30
katika soko. Sekta ya bima kwa upande wa kuenea kwa usajili imekua
kwa kiwango cha asilimia 0.7 ya Pato Ghafi la Taifa (GDP) kwa mwaka 2015. Katika
kipindi hicho bima ya maisha
ilichangia shilingi bilioni
0.3.
Mwaka
2014 kiwango cha jumla kilipanda kwa asilimia 17 hadi kufikia shilingi bilioni 554.4 kutoka shilingi
bilioni 474.1 kwa mwaka 2013. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima
Tanzania (TIRA) kiwango cha bima zilizokatwa
nchini kilipanda kwa
asilimia 76 hadi 12,052/- mwaka 2014 kutoka 6,849/- mwka 2010.
Sekta
hii inakadiriwa kukua kwa asilimia 18 kwa mwaka 2016 na kupenyeza kwa
bima kufikia asilimia 0.9
ya Pato Ghafi la Taifa (GDP). Kwa mujibu wa shirika
maarufu la bima duniani Swiss Re ni kwamba Afrika Kusini ambayo ni nchi iliyo
na uchumi mkubwa barani Afrika haishangazi
kwamba ilichangia asilimia
75 au dola za Marekani bilioni 51.6 ya bima zote barani humo kwa mwaka 2013.
Mugo
alibainisha kwamba sekta ya ndani ya bima inakua kwa kasi akisema
kuwa kuingia kwa wadau wengi katika soko kutasababisha
uwepo ushindani wa kupata nafasi ndani ya sekta hiyo yenye faida. “Ushindani ni
mzuri katika biashara”, alisema Mugo na kuongeza, “ni kwa kuwa kila mara inapokua ni wito wa
kuzindua biashara ili iwe na ubunifu zaidi na uanzishwaji wa bidhaa kunakowapa wateja huduma bora na nzuri.”
Ikiwa
inakadiriwa kwamba mapato ya jumla yanayotokana na biashara ni zaidi ya silingi bilioni 10.0, RI inajivunia
kuwa na watoaji huduma zaidi
ya 300 kote nchini na waajiri zaiidi ya 80 inaonesha dhahiri kuwa ni moja ya
mchangiaji mkubwa katika
sekta ya bima ndani ya nchi.
No comments:
Post a Comment