Chama cha ADC kimemwomba Rais Magufuli katika miaka hii mitatu iliyobaki kubadilisha msimamo wa kuzuia kufanywa kwa mikutano ya hadhara inayotakiwa kufanywa na vyama vya upinzani.
Akizungumza katika kuelekea maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa chama hicho Katibu mkuu wa chama cha ADC , Doyo Hassan Doyo amesema wao wanania nzuri ya kufanya siasa nakusema Rais asione kwamba vyama vyote vinakauli mbovu katika kufikisha ujumbe kwa jamii.
Doyo amesema suala la Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa vyama vingine vya Demokrasia na kusema wao hawana mbunge wala diwani hivyo wana ufinyu mkubwa wa kufanya siasa, na kusema kuwa wao wanapaswa kufanya siasa kwa nguvu zote ili kuongeza wananchama na hatimae kujipatia viti vingi vya uongozi.
"leo umezuiwa kusema inamaana hutoweza kupata sapoti ya watu na watu hawatoweza kufahamu sera za chama chako kutokana kutoweza kufanya mikutano ya kisiasa" Alisema Doyo.
Aidha Chama hicho kinafanya maadhimisho hayo kwa njia ya ziara ambapo watatembelea baadhi ya taasisi za kidini,magereza ,hospitali,pamoja na vyombo vya habari.
Ziara ya chama hicho imeanza leo katika katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam lakini hawakupata fursa ya kukutana na mkuu mkoa huyo Paul Makonda kutokana na kuwa nje ya ofisi.
Hata hivyo chama hicho kimefanya jitihada ya kuwasiliana na mkuu huyo na kuwaahidi katika ratiba zao zinazoendelea waweze kuwasiliana nae ili waweze kuzungumza kama ilivyo kusudiwa.
No comments:
Post a Comment