Wednesday, July 19, 2017

ADC WAMCHARUKIA TUNDU LISSU KWA KAULI ZAKE

Ndugu waandishi wa Habari, 
  Habarin za Leo, 
Jana katika baadhi ya vyombo vya Habari, tumemsikia mwanasheria mkuu  wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA MH, Tundulisu, 
   Akizitaka jumuiya za kimataifa kuzifutia misaada mbali mbali ambayo inaisaidia nchi yetu, 
 Chama chetu cha alliance for democrat change ADC dira ya mabadiliko kimestushwa na kauli hiyo ya kinyama Kabisa Kwa watanzania, 
 ADC inataka chadema itoe Tamko LA kuwa ile kauli aliyoitoa mwanasheria wa chadema ni ya chama au ni yakwake binafsi, 
CHADEMA iwaombe radhi watanzania Kwa kitendo chake cha kutaka watanzania waondolewe misaada yakibinadamu, 

ADC imestushwa na unyama huo wa chadema yakutowatakia  watanzania mambo mema, 

Madai ya kuwa nchi haindeshwa kidemocrasia huo ni mtazamo wake japo yeye ni Mbunge aliyetokana na Uchaguzi wa kidemocrasia, 
Na kuhusu udicteta wa mh, magufuri Kwa Maoni yake, haituondelei sisi watanzania wengine kupata misaada ya kibinadamu,  
 
ADC inaamin mapambano ya ndani tukijipanga vizuri tutayashinda majaribu yote yaliyoko mbele yetu katika nchi yetu. 

Tunadhan matatizo yetu ya ndani ni vema tukapambana nayo kuliko kutangazia ugomvi wako mtu asiyekuhusu huu nao ni udhaifu mkubwa wa Kiongozi, 




Kwa mtu aliye makini na anayejua anachokifanya kamwe ugomvi wake wa ndani hawezi kuupeleka nje ya mtu mwengine, 

Kwa kauli hizi za Chadema ni wazi wameshindwa mapambano ya ndani  na sasa wanafikiri njia nyingine ambazo ni hatari zaidi katika nchi yetu, 

Tunaiomba serikali kuzipima kauli za chadema katika uzito unaostahili la sivyo chadema wanaweza kuja kuitia nchi katika matatizo yasiyokuja kuzuilika,. 

Tunaishauli Chadema Kama wameshindwa kupambambana na CCM na serikali yake ni wazi wawaeleze wafuasi wao kuliko kutoa matamshi ambayo yanaweza kuhatarisha ustawi wa Taifa letu, 


Mwisho... 

Tunawaomba watanzania wote kuyapuuza maneno ya mwanasheria mkuu wa chadema na msimamo wa chama chake wa kutaka Tanzania ifutiwe misaada, 

Nawatakia siku njema 


Mungu IBARIKI ADC, 

Mungu IBARIKI TANZANIA, 

ADC dira ya mabadiliko, 

Imetolewa na 

Mh Doyo Hassan Doyo 

Katibu Mkuu 
Alliance for democrat change (ADC)

No comments: