MBALARI, MBEYA: Watu wawili wamefariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria la kampuni ya Upendo kuacha njia na kupinduka eneo la Malimboji-Igawa wilayani Mbalari.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Augustino Senga amesema ajali hiyo imetokea leo (Julai 6) saa 2:15 asubuhi.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva ambaye alikimbia baada ya ajali kutokea. Basi hilo lilikuwa likitoka Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Senga amewataja waliokufa kuwa ni Emmanuel Obeid mkazi wa Chimala mkoani Mbeya na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Shahib, mkazi wa jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment