Afisa
Sheria Bi. Doris Mugarula (wakwaza kushoto) na Afisa
Fedha Bi. Happiness Kisanga (wapili kushoto) wa Benki ya KCB wakimsikiliza mjasiriamali Bi. Batula akielezea maendeleo ya
biashara yake ya nguo mkoani Arusha.
Afisa
Masoko wa Benki ya KCB Bi. Ghati Muhere (kulia) akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Hafsa Ali
(kushoto) katika duka lake la nguo za kiume, H&D Collection Shop, Kariakoo,
jijini Dar es Salaam.
Afisa Sheria, Bi. Doris Mugarula (wakwanza kulia) na Afisa Fedha
Bi. Happiness Kisanga (wapili kulia) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Shamsa Ally
(kushoto) katika duka lake la vifaa vya magari makubwa mkoani Morogoro.
Afisa
Fedha wa Benki ya KCB Bi. Happiness Kisanga (wakwanza
kulia) akimpatia ushauri wa kibiashara
mjasiriamali Bi Hawa Mabrouk (katikati) katika ofisi yake ya Video production,
Ilala, jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko, wa Benki ya KCB, Bi. Ghati Muhere (kulia), akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Jac Bazaar (kushoto) katika duka lake la vifaa vya umeme mkoani Morogoro |
Afisa
Masoko Bi. Ghati Muhere (aliyechuchumaa) na Afisa
Fedha Bi. Happiness Kisanga (aliyesimama) wa Benki ya KCB wakimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Violeth
(aliyeinama) katika biashara yake ya kilimo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Afisa
Masoko wa Benki ya KCB Bi. Ghati Muhere (kushoto) akimpatia ushauri wa kibiashara mjasiriamali Bi Selina (kulia)
katika duka lake la bidhaa za watoto Jijini Mwanza.
Afisa
Sheria wa Benki ya KCB Bi. Doris Mugarula (kushoto) akimsikiliza mjasiriamali Bi Fatma (katikati) akielezea
kuhusu biashara yake ya vipodozi na mikoba ya kike Jijini Mwanza.
KCB 2jiajiri ni programu inayolenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika matatizo yanayosababisha biashara yake ishindwe kukua na kuwa endelevu. Matatizo yanayolengwa kutatuliwa kutoka kwa wanawake wajasiriamali hawa ni elimu ya kifedha, kufikiwa na huduma za kifedha, ukosefu wa dhamana, kutokujua vizuri masuala ya kisheria, uelewa finyu wa sera za serikali na kiuchumi, njia hafifu za kuendesha biashara endelevu, ukosefu wa mtaji, utaalamu wa kuanzisha biashara kubwa n.k.Benki ya KCB Tanzania inaendelea kuwapatia wanawake wajasiriamali waliopitia mafunzo ya ujasiriamali ya KCB 2jiajiri ushauri wa kibiashara kwa vitendo ofisini kwa wafaidika wa 2jiajiri. Maafisa watatu ambao ni; afisa fedha, sheria na masoko wanawatembelea wafaidika hao wajasiriamali waliomaliza mafunzo ya KCB 2jiajiri katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Morogoro na Zanzibar.
“Programu
hii ilizinduliwa
rasmi Desemba, 2016, ambapo hadi sasa tumewapa stadi za biashara endelevu
wanawake wajasiriamlai 258 kutoka mikoa 6 ya Tanzania.” Alisema Christine
Manyenye, Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB.
Akielezea kuhusiana na programu ya KCB 2jiajiri Bi. Manyenye
alieleza kuwa, wafaidika wa KCB 2jiajiri baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu
darasani, kwa sasa wananufaika kwa kupata ushauri wa kibiashara na kitaalamu kutoka
kwa washauri watatu katika nyanja za Kifedha Kisheria na Masoko.
aliishukuru Benki ya KCB kwa kutoa mafunzo ya kibiashara
ambayo yamepanua ufahamu wa jinsi yakuendesha biashara. “kupitia KCB 2jiajiri
nimeweza kujua umuhimu wa kurasimisha biashara, kuwa na leseni ya biashara,
kuweka kumbukumbu katika biashara na jinsi ya kuendesha biashara kiujumla”
alisema Bi. Kipangula.
Benki
ya KCB kimsingi inatambua mchango mkubwa wa wanawake wanaoutoa katika sekta
binafsi hususani katika Ujasiriamali mdogo na wa kati (SMEs) hivyo lengo kwa
ujumla ni kuwezesha wafanyabiashara wanawake wa Kitanzania kuandaa mikakati
ambayo inaboresha stadi zao na uwezo hivyo kuunda fursa nyingi za kibiashara
kwa ajili yao.
Bi.
Manyenye alimaliza kwa kusema kuwa programu ya KCB 2jiajiri ni endelevu na kwa
wanawake wajasiriamali ambao bado hawajajiunga na KCB 2jiajiri wajiulize kwa
nini wahangaike wakati KCB 2jiajiri ipo kwa ajili yao.
Kuhusu
Benki ya KCB
Benki ya KCB
ni benki kubwa zaidi katika Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka
1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za
Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii
ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi zaidi ya 250, mashine
za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 13,562.
KCB Bank Group pia inamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB
Capital na KCB Foundation.
Nchini Tanzania, KCB
ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika
kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi,
Lumumba ,Buguruni, Oysterbay, Pugu jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar,
Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro
No comments:
Post a Comment