Shindano la
mchezo wa mpira wa kikapu kwa wafanyakazi wa benki lijulikanalo kama Brazuka linatarajiwa kushirikisha benki saba tofauti hapa nchini.
Akitoa taarifa hiyo kaimu katibu mkuu wa chama cha mpira wa kikapu hapa nchini(TBF) Bw. Michael Mwita amesema mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe
15 mwezi huu katika viwanja vya Uhuru, JMK Park na Gymkhana ambapo jumla ya benki saba zimethibitisha kushiriki katika mashindano.
``Mpaka sasa kuna jumla ya benk saba amabazo tayari zimethibitisha kushiriki mashindano haya kitaifa na mpaka sasa bado tunazidi kutafuta wadhamini ilikusapoti mashindano haya ya kibenk``alisema
Aidha, meneja masoko wa benki ya
NMB,
Bw Yusuph Shenyagwa alithibitisha kushiriki mashindano hayo huku akizitambia benki pinzani ikiwemo ya Stanbik ambapo ili wakilishwana
Captain wa timu hiyo Bw. Peter
Bahema nakuwa wataweza kuibuka washindi wa mashindano hayo maana wanauzoefu wakutosha na mashindano hayo hivyo watapambana kwa hali yoyote kuhakikisha wanaibuka washindi.
Pia, Mratibu wa mashindano hayo ya Brazuka Kibenk, Bi. Nasikiwa Berya amesema maandalizi yote yanayohusiana na mashindano yamekamilika nashindano hilo litakuwani
la
kitaifa kwani wanataka watumishi wa kibenki wapate fursa ya kushiriki michezo kwani itawajenga kiafya nakuzidi kujenga mahusiano mazuri kati ya benki na benki.
``Mashindano haya yatajumuisha benki saba na jumla viwanja vitatu vitatumika katika michezo hiyo kukiwa na hatua tatu tofauti yaani mtoano, nusu fainali na
finali yenyewe itakayopigwa siku ya mwisho ya michuano hiyo`` alisema mratibu.
Mashindano hayo yana tarajiwa kuanza tarehe 15
mwezi huu hadi 29 ambapo benki saba zikiwemo NMB, DTB, CRDB, BOT, STANBIC, ABC
na BARCLAYS zinatarajiwa kushiriki na mshindi kuondoka na Kombe pamoja na medali
No comments:
Post a Comment