Tuesday, July 4, 2017

DC HAPI - HALIMA MDEE AKAMATWE MARA KWA KOSA LA UCHOCHEZI

Leo July 4, 2017 saa 5 asubuhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi alitoa agizo la kukamatwa kwa Mbunge wa Kawe Halima Mdee na kuwekwa Polisi kwa saa 48 baada ya kudaiwa kutoa kauli za kichochezi kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya CHADEMA.

DC Ally Hapi alisema:>>>”Kauli ambazo alinukuliwa akizizungumza Halima Mdee zina matamshi ambayo ndani yake yamelenga kumfedhehesha Rais. Kauli ambazo zimelenga kuleta uchochezi kwa Rais wetu ambaye ndiye kiongozi mkuu wa Nchi, Serikali na Amir Jeshi Mkuu.
“Katika mazungumzo yake Mdee ameeleza kwamba ‘Rais amekuwa na tabia ya ovyo na kwamba tabia hiyo imempelekea kuona maneno yake ndiyo sheria ya nchi.
“Kwa Mamlaka niliyo nayo, kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa, kifungu Namba 15 naagiza Halima Mdee akamatwe na Jeshi la Polisi, awekwe ndani kwa masaa 48 kwa mujibu wa Sheria, ahojiwe na afikishwe katika vyombo vya kisheria ili aweze kurusaidia kujibu matusi haya ambayo ameyatoa dhidi ya Rais wetu.” – DC Ally Hapi.

No comments: