A CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ametoa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wa vizimba vya standi ya mabasi Ubungo kulipa kodi na kusisitiza kuwa iwapo watakaidi agizo hilo, ataagiza Polisi kuwaondoa kwa nguvu.
Mstahiki Meya Mwita ametoa agizo hilo leo alipofanya ziara ya kushtukiza katika standi ya mabasi ya Ubungo ikiwa ni baada ya kupokea taarifa kuwa kuna wafanyabiashara hawataki kulipa kodi.
Katika ziara hiyo Meya Mwita aliambatana na Kamati ya Fedha na uchumi ya jiji ambapo kabla ya kutoa maamuzi hayo, a litoa nafasi kwa wafanyabiashara kuzungumza kuwa ni kwanini hawataki kulipa kodi , na hivyo baada ya kupokea maelezo hayo alifikia hatua ya kutoa maamuzi hayo.
Meya Mwita alisema kuwa jambo la wafanyabiashara hao kugoma kulipa kodi ambazo wanapaswa kulipa, ni kulikosesha jiji mapato ambayo yangeweza kutumia kwenye shughuli za Maendeleo na kusisitiza kuwa wasitake kuingia kwenye mgogoro na jiji.
" Ndugu zangu sasa mmeanza kunipa wasiwasi mkubwa, lakini pia mnataka kunilazimisha nitumie utaratibu wa kutangaza tenda zakuingia humu ndani kufanya biashara zenu, jambo ambalo kwa silimia 100 najua hamtapata, na wote hapa mnategemea kupata chochote hapa, sasa msitake nifike huko.
Hizi pesa ambazo mnalipa hapa, ndio zinatumika kufanya usafi hapa, lakini pia pesa hizo hazina kazi moja tu, sasa mkisema hamtaki kulipa mnataka hii stendi hapa ijiendeshe vipi?, sasa naagiza hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa nane, muwe mmeshalipa kodi, vinginevyo polisi watawaondoa hapa.
Alisisitiza kuwa, msije kushangaa, hapa Polisi wanawaondoa kwa nguvu, na polisi Ikifika muda huo ambao nimeutoa halafu ikatokea pesa hazijalipwa, hawa watu hapa nisiwaone"aliagiza Meya Mwita.
Hata hivyo katika hatua nyingine aliwataka watumishi wa standi ya Ubungo kuwa na kauli nzuri kwa wafanyabiashara sambamba na kuonyesha ushirikiano huku pia akionya wafanyabaishara namkuwataka waonyeshe ushirikiano kwa watendaji walipo kwenye standi hiyo.
No comments:
Post a Comment