Sunday, July 9, 2017

Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka

Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi usiku wa Julai 8,2017, amezindua rasmi tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), tukio lililofanyika Ngome Kongwe, Mjini Unguja-

Zanzibar. Katika tukio hilo, Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo la 20, tokea kuanzishwa kwake miaka 20, iliyopita. Ambapo uongozi wa ZIFF waliweza kusoma wasifu wa Rais huyo Mstaafu kwa namna alivyoweza kusaidia mchango mkubwa kuendeleza tasnia ya filamu nchini na sanaa kwa ujumla huku akiwa ndio kiongozii wa juu kabisa hapa nchini kuizungumzia mara kwa mara tamasha hilo la
 ZIFF. 
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmo, Dkt. Jakaya Kikwete alishukuru na kupongeza kwa mafanikio waliyopata ZIFF hadi kufikia msimu wa 20, tokea kuanzishwa kwake ambapo imewataka waendelee zaidi na zaidi. “Nashukuru kwa kunialika. Nashukuru kwa tuzo hii kwani sikutegemea na nina wapongeza kwa mafanikio haya ua kutimiza miaka 20. Nawaombeeni muendelee miaka 20 na 20 zaidi vizazi na vizazi mpaka litakapofika mwisho” alieleza Dkt. Kikwete. Dkt. Kikwete alitoa ushahuri kwa uongozi wa ZIFF kuwa na kifua mbele kwa namna filamu zinazopita kwenye tamasha lao kuzifuatilia kwani zimekuwa zikifanya vizuri huko mbele ikiwemo tuzo za Hollywood. Kwani ZIFF imekuwa ni taasisi yenye nafasi muhimu kwa jamii ya watu wa Zanzibar Tanzania . Kwa sasa ni kujipima katika miongo miwili hii ni jinsi gani na kiasi gani ZIFF ilivyojisogeza na kuwa karibu na jamii” alieleza Dkt. Kikwete. Aidha, Dkt. Kikwete alieleza kuwa, tasnia ya sanaa hapa nchini inatakiwa ipande na kuwa juu ili kuendeleza utamaduni wa Mzanzibar na Mtanzania inaenda vipi. 

Pia amewataka ZIFF kuwa karibu na jamii ili kuweza kujenga ushawishi kwa jamii hiyo na kilamwaka wawe na matamanio zaidi ya tamasha. Awali akitangaza tuzo hiyo, Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo mbele ya jopo la wajumbe wa Bodi ya ZIFF, waliweza kumtangaza rasmi Dkt. Kikwete kutwaa tuzo hiyo kubwa kabisa ambayo utolewa kwa watu wenye kutukuka ambao pia wameifanya mchango mkubwa ndani na nje katika masuala ya Sanaa na tasnia ya filamu. Mwenyekiti wa ZIFF Mahmoud Thabit Kombo aliweza kuwataka wazawa hasa Wazanzibar kuwa na mwamko wa kuthamini cha kwao na hata kujitokeza kudhamini tamasha hilo. “ZIFF imefungua milango yake wazi kwa mtu yeyote kujitokeza na kudhamini tamasha hili. Wazawa tunawakaribisha sana kwani uwepo wa tamasha ili ndio kukuwa kwa uchumi wetu na maendeleo hivyo tujisikie fahari kwa uwepo wake”. Ameeleza Mahmoud Thabit Kombo. Akiwa mgeni rasmi, Dkt. Kikwete aliweza kushuhudia filamu ya uzinduzi wa tamasha hilo ya ‘T-Junction’ iliyoandaliwa na mtayarishaji wake Amir Shivj kutoka Kijiweni Production ya Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo, Ngome Kongwe iliweza kufurika umati mkubwa waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo. Imeelezwa kuwa, wageni kutoka mataifa mbalimbali zaidi ya 14,000 wamefika Visiwani Zanzibar huku hoteli mbalimbali zikiwa zimepata faida kwa kipindi hiki, alieleza Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. 

Mahmoud Thabit Kombo ambapo ameweka wazi kuwa katika orodha yao ya wageni kutoka Mataifa mbalimbali huku wengine wakiendelea kufika kila siku. Tamasha hilo linatarajia kumalizika hadi Julai 16,2017. Huku kila siku kukiwa na filamu zinazoonyeshwa Ngome Kongwe na zingine zikioneshwa kwenye kumbi mbalimbali ndani ya viunga vya Unguja pamoja na Vijiji vya Zanzibar sambamba na kutoa mafunzo ya uendeshaji wa filamu na mafunzo mbalimbali katika tasnia hiyo ya filamu. Imeandaliwa na Andrew Chale, MO BLOG-Zanzibar
Mkurugenzi wa ZIFF, Daniel Nyalusi (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Zanlink wakipata picha wakati wa ufunguzi huo wa tamasha la ZIFF 2017, ambalo kwa mwaka huu ni la 20, tokea kuanzishwa kwake.
Wadau mbalimbali wa wakipata picha wakati wa ufunguzi huo wa tamasha la ZIFF 2017, ambalo kwa mwaka huu ni la 20, tokea kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi wa zamani wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Busara Promotion ambao ni waandaji wa tamasha la Muziki la Sauti za Busara, Yusuph Mahmoud ama 'Dj Yusuf'
wadau wakiwa kwenye picha ya kumbukumbu
Mwendesha kipindi cha senema zetu akiwa 'mbashara' wakati wa ufunguzi huo
Mmoja wa wageni waliofika kwenye tamasha hilo ambapo alikuwa kivutio kwa muonekano wake wa kama aliyeigiza filamu ya YESU " JESUS'
Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. Mahmoud Thabiti Kombo akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa ZIFF, Daniel Nyalusi wakati wa uzinduzi huo
Mmoja wa wadau wakubwa wa tasnia ya filamu na muziki hapa nchini Dada Sauda Simba akihojiwa 'mbashara' na kipindi cha SINEMA ZETU
Wadau mbalimbali wakipata picha ya ukumbusho kwenye zuria jekundu
wadau wakipata kumbukumbu
Mkurugenzi wa Fabrizio Colombo akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Busara Promotion ambao ni waandaji wa tamasha la Muziki la Sauti za Busara, Yusuph Mahmoud ama 'Dj Yusuf'
Burudani ikiwendelea
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa ZIFF, Profesa Martin Mhando
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi wageni waalikwa wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongzi wengine wakipiga makofi kupongeza bendi iliyokuwa ikitumbuiza
upande wa viongozi na wagei waalikwa wakifuatilia tukio hilo
Wakurugenzi wapya wa ZIFF wakitambulishwa katika ufunguzi huo, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF Daniel Nyalusu na kushoto ni Mkurugenzi wa ZIFF Fabrizio Colombo
Mkurugenzi wa ZANLINK akizungumza katika tamasha hilo
Burudani
Mwenyekiti wa ZIFF 2017, Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha mgeni rasmi Dkt. Kikwete jukwaani
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshika tuzo yake hiyo ya mtu aliyetukuka wa ZIFF baada ya kukabidhiwa na Bodi ya ZIFF usiku wa Jumamosi Julai 8,2017. Ngome Kongwe, Unguja
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika tukio hilo
Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatilia filamu ya T-Junction ya Amri Shivji iliyokuwa ikifungua tamasha hilo
Dkt. Kikwete akiselebuka pamoka naMkurugenzi wa ZIFF, Fabrizo Colombo pamoja na kikundi cha Mwandege wakati wa tukio hilo la ufunguzi wa tamasha la ZIFF la 20
Mkurugenzi wa ZIFF, Fabrizo Colombo akizungumza katika tukio hilo
Amir Shivj wa Kijiweni Production akitambulisha 'crew' yake ya wasanii walioigiza katika filamu ya T-Junction.
Picha zote na Andrew Chale-MO BLOG, Zanzibar

No comments: