Friday, July 14, 2017

TANAPA YAMPATIA DK JANE GOODALL TUZO YA UTAFITI WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE TANZANIA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi  Dk. Jane Goodall tuzo maalumu kwa kutambua mchango wake wa utafiti wa miaka 60 wa maisha ya Sokwe  pamoja na uhifadhi wa wanyama wengine kwenye hifadhi ya Gombe, mkoani Kigoma  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Tuzo hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa). Habari zaidi zitaletwa punde.


Na Richard Mwaikenda

Jane ambaye ni raia wa Uingereza alianza utafiti katika Hifadhi ya Gombe mnamo miaka ya 60 akiwa na umri wa miaka 26.



Katika utafiti wake amegundua mambo mengi ikiwemo jinsi Sokwe wanavyojitambua, kuwa na hisia na jinsi wanavyoishi kwa ushirikiano kama walivyo binadamu.




Akizungumza katika hafla hiyo jane anasema wakati anaanza kufanya utafiti ilikuwa vigumu Sokwe hao kumkaribia kwani walikuwa wanamuogopa na ilikuwa ni mara ya kwanza kwao kumuona mtu mweupe, lakini alifanya jitihada hadi wakamzoea na kuanza kumsogelea na kumuona mtu wao wa karibu.




Anasema alitumia mbinu mbalimbali kama vile kuwapatia ndizi na vyakula vingine hadi wakamzoea.




Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Utalii katikati ya jiji la Dar es Salaam, viongozi na wageni waalikwa walipata wasaa wa kuangalia picha mbalimbali za matukio ya sokwe wakiwa na Jane Goodall.




Katika utafiti wake amefanikiwa kuanzisha chuo na kutunga vitabu pamoja na video zinazoelezea maisha yake na Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma.




Katika hafla hiyo walihudhuria Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali George Waitara, Mwanasiasa Mkongwe, Getrude Mongela, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Goodall, Lembeli, Balozi wa Uingereza nchini, mabalozi mbalimbali pamoja na waalikwa.

Dk. Jane akikabidhiwa cheti cha kutambua mchange wake kwa Tanzania kwa kuhifadhi Sokwe na wanayama wengine

 Jane akipatiwa pia zawadi ya kinyago cha Sokwe
 Jane akikabidhiwa picha ya Sokwe
 Mama Mongela akimvisha Jane zawadi ya vitenge
 Dk Jane akitoa maelezo kuhusu maisha ya Sokwe
 Waziri Maghembe akipata maelezo kuhusu maisha ya Sokwe yalivyo
 Wasanii wa Tanapa wakitumbuiza kwa wimbo 


 Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Mjeshi Mstaafu, Jenerali Waitara akitoa shukrani nyingi kwa Dk Jane kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuiletea Tanzania sifa lukuki duniani
 Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini wakati Waziri Maghembe akihutubia katika hafla hiyo, ambapo alisema kuwa Dk. Jane ambaye wakati anaaza utafiti yeye alikuwa darasa la pili, lakini utafiti wake umeiletea sifa kubwa Tanzania na utakuwa ni urithi wa kipekee maishani
 Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini

 Profesa Magembe akihutubia katika hafla hiyo ya kumpatia tuzo Dk. Jane
 Baadhi ya mabalozi waliohudhuria hafla hiyo
 Dk Jane akielezea historia yake na jinsi alivyofanikiwa kufanya utafiti huo wa sokwe


 Lembeli akitoa neno la shukrani
 Jane akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi waliohudhuria hafla yake pamoaja na viongozi mbalimbali


 Jane akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari baada hafla kumalizika

No comments: