Wazazi kote nchini wanatakiwa kuwa waangalifu na wapende
kuwachunguza watoto wao nyendo zao wawapo majumbani na pia waendapo mashule. Hayo
yamesemwa jana kwenye semina iliyofanywa na mtandao wa jinsia Tanzani(TGNP) lengo
likiwa ni kuwapa elimu wakazi wa Tandika ili kupinga ukatili wa kijinsia unaofanywa
kwenye maeneo yanayowazunguka.
Baadhi ya wakazi wa Tandika wakiangalia sinema ya kuelimisha ili kujifunza mambo mbalimbali ya ukatili wa kijinsia mapema jana jijini Dar es salaam |
Kupitia semina hii imeonyesha kuwa eneo la Tandika
linaukatili wa hali ya juu wa kijinsia unaotekelezwa na wanaume wa kata hiyo. Baadhi
ya wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa mapaka leo hii kuna baadhi ya wazazi
wakiume wanakataa kuwapeleka watoto wao wa kike shuleni kwa madai ya kuolewa.
Baadhi ya wakazi wa Tandika wakimsikiliza kwa makini muwezeshaji wa semina toka TGNP Mtandao Bw. Speratus Kyruzi kwenye semina iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam |
Akitoa ushuhuda Bi. Khadija Ramadhani alisema kuwa yeye
jirani yake aligoma kumpeleka shule ya sekondari mtoto wake wa kike kwa kudai kuwa
ameshafikia umri unastahili kuolewa. Na kusema kuwa mpaka sasa ameshatolewa barua na inasubiliwa
ndugu wa pande zote mbili kuelewana kwa pamoja ili aweze kuozeshwa kwa kuwa ameshachezwa ngoma na
umri wake unatosha kabisa kuolewa kwa kuwa ameshatimiza miaka 14.
Kulawitiwa kwa watoto wakiume na miongoni mwa matatizo
kwenye kata hiyo ya Azimio baadhi ya wakazi wa kata hiyo wakiomba msaada
kupitia taasisi na serikali kwa ujumla kuliangali swala hilo kwa umakini zaidi.
Bi. Sharifa Hassani akiongea kwa jazba pindi alipokuwa akitoa maoni yake kwenye semina ya kupinga ukatili wa kijinsia mapema jana jijini Dar es salaam |
Bi. Sharifa Hasani ni miongoni mwa waanga wa tatizo hilo kwa
kusema kuwa yeye mwenyew mtoto wa kaka yake ambaye alirubuniwa na mbaba mtu mzima
ambaye ni mkazi wa Temeke . Huyo jamaa alikuwa akienda kumchukua shuleni bila walimu na wazazi wake kufahamu
na hivyo kuja kugundua ikawa tayari mtoto amelawitiwa kwa muda mrefu ameshaharibika,
Na walipojaribu kuulizwa walimu wanasema ana miezi mtoto ajaonekana darasani
ndipo kuja kufanya uchunguzi walimgundua mualifu na mpaka sasa yupo chini ya
polisi kwa kosa alilolifanya.
Tatizo la ubakaji pia lipo kwa asilimia kubwa kwa mabinti wa eneo hilo, kubakwa mabinti na ndugu zao hata wazazi kubaka
watoto wao.
Pili Mkologo yeye alishudia kwa baba aliyemfukuza mkewe na
kubaki na watoto wake wakike watatu ambao baadae baba huyo aliamua kuwatumia
kama wake zake aliamua kutembea na mwanae mkubwa na bado akaona haitoshi
akaamua kutembea na wote mapaka wa mwisho ambae alikuwa ni mdogo sana kwa
kuwapa vitisho vya kuwaua endapo watasema yanayoendelea ndani mwao. Na baadae mama
kuja kugundua alichokifanya mumewe ikawa muda umeshapita kashawaharibu watoto
wote.
Bi. Tatu Khamisi Kitenge akitoa maoni yake kwenye semina ilifayika mapema jana jijini Dar esa salaam |
Lakini pia kuna familia ambayo pia wazazi walishindwa
kuendesha kwa maadili mazuri na mama alikuwa anapika ugali na kila mtoto anaambiwa
akajitafutie mboga. Hali hii ikamfanya binti yao ambae alikuwa anasoma kuweza
kushawishiwa na babu yake ambae ni mzazi wa mama yake kwa kumpa pesa za
kununulia chipsi, kuku na baadae wazazi walipogundua walimpeleka polisi. Na baadae
walimalizana kifamilia na Yule mzee akaachiwa na kuondoka zake pasipojulikana.
Lakini pia tatizo lingine ni katika swala la ugawanaji wa
rasilimali bado ni tatizo kwa kuwa kuna mama kwenye kundi hilo waliweza
kushirikiana kwa pamoja na mumewe kutafuta mali yeye akiwa anauza vitumbua na
mumewe anauza samaki lakini walipogombana mwanamke alikatazwa asiondoke na
chochote na vitu vyote vikawa mali ya mwanaume.
Mimba za utotoni vimeshamili kwa kiasi kikubwa na hatimae
kuweza kuunda kikundi kinachoitwa "Umoja wa Mama Wadogo" yani umoja huu
unawahusisha wale watoto waliozaa wakiwa na umri usiostahili kuzaa ambao ni chini ya miaka 18.
Mdau wa watoto kata ya Amani bw. Juma Tetele akitoa mchango wake kwenye semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) mapema jana jijini Dar es salaam |
Na mwisho kabisa mdau wa watoto toka kata ya Amani Bwana
Juma Tetele alisema kuwa yeye mpaka sasa ana kesi mbili anazozisimamia za
ulawiti wa watoto na kuwaomba wazazi wawe makini na watoto wao wawapo nyumbani
na pia waendapo shuleni. Aliwaomba wazazi
ikiwezekana wachukue mawasiliano ya simu kwa walimu ili kupewa taarifa kuhusu maendeleo
ya watoto pia wakirudi nyumbani wawena tabia ya kuchunguza walichokifanya
shuleni kwa siku hiyo.
Na jambo lingine aliwaomba wazazi kutopendelea kuwaweka
vijana wao wadogo na wageni ambao ndugu zao au sio ndugu bila kufahamu tabia
zao vizuri, kwani hii inakuwa ni miongoni mwa sabababu za kubakwa au kulawitiwa
kwa watoto hao.
Wakazi hao pia waliomba mashirika mengine yanayotetea haki
mbalimbali yaweze kuiga mfano wa TGNP wa kuwafuata wananchi na kuwapa elimu na
sio kukaa maofisini na kusema tu wao ni wanaharakati." Wanaharakati ni kujitoa
kujua wananchi wanachangamoto gani ili kuweza kuwasaidia kuzitatua sio mapaka
waje ofisini kwako ndio ujue kuna watu wanashida za kisheria".walisema wakazi hao
Lakini pia wazazi wakike kwa wakiume wametakiwa kukaa na
watoto wao wakike kwa wakiume kuwapa elimu ya afya ya uzazi ili kupunguza
tatizo la mimba za utotoni na ubakwaji kwa watoto wao wa kike.na ulawiti kwa
watoto wa kiume. Na kuwaeleza nini cha kufanya kabla madhara hayo kutokea.
No comments:
Post a Comment