TGNP Mtandao bado inaendeleza semina zake za kutembelea kata
mbalimbali za jiji la Dar es salaam lengo likiwa ni kuwapa elimu wakazi wa kata
husika juu ya kupinga ukatili wa kjinsia uliopo kwenye kata zao. Leo ikiwa ni
siku ya tarehe 3 julai wawezeshaji toka
TGNP mtandao walitembelea kata ya Mburahati na kuongea na wakazi wa eneo hilo
kwenye ukumbi wa Baba Watoto uliopo Mburahati jijini dar es salaam.
Bw. Selemani Shabani akichangia hoja kwenye semina ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika Mburahati mapema leo jijini Dar es salaam |
Mila na Desturi potofu zimekuwa ni miongoni mwa sababu
zinazopelekea kuwepo kwa mimba za utotoni kwa kuwa inaeleweka kuna baadhi ya
makabila watoto wakifikia umri wa miaka 12 wanapelekwa kwenda kuchezwa ngoma na
huko hakuna kinachofundishwa zaidi ya kumjua mwanaume na jinsi ya kumtumia ni
siyo mafunzo mema ambayo yatamjenga mtoto huyo kwa maisha ya baadae.
Bi. Amina Omary akichangia mada kwenye semina ya kupinga ukatili wa kijinsia, mapema leo jijini Dar es salaam |
Pia imeelezawa kuwa baadhi ya wazazi wa eneo hilo
wanashindwa kuyabeba majukumu yao kama wazazi hali inayosababisha watoto wao kupotea ki maadili.
Kutokana nan hili uanakuta mzazi anashindwa kukemea tabia ya mtoto wake kwa
kuwa binti huyo huyo akipata pesa toka kwa wanaume wake anampatia na mama
anaongezea kwenye pesa ya chakula hali inayofanya mzazi wake wa kike asiwe na
sauti kwenye hili.
Bw. Yahaya Konde akichangia hoja kwenye semina iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam |
Na wazazi kuwa wakali kupita kiasi ni miongoni mwa sababu zinazomnyima
mtoto haki yake ya msingi hivyo unakuta hata kama mtoto anateswa na mzazi mmoja
wapo anashindwa kuongea na mzazi wake kwa sababu ya ukali wake mtoto anakosa
mshauri hali inayosababisha mtoto kufuata ushauri wa marafiki au watu wengine
wabaya hivyo kuingia kwenye makundi mabaya. Hii imeelezwa kuwa ni sababu
ilifanya kuharibika kwa vijana wa eneo hilo.
Bi. Benadetha Mwale akitoa maoni yake kwenye semina ya kupinga ukatili wa kijinsia mapema leo jijini Dar es salaam |
Tatizo la kupigwa kwa wamama nalo lipo kwa kiasi kikubwa
kutokana na makosa ya watoto wao au ya kwao wenyewe, hii imeelezwa kuwa wamama
wengi wanapigwa na kushindwa kutoa taarifa juu ya uonevu uliopo kwa kuogopa
kupoteza ndoa zao, hivyo upewa kipigo na asubuhi anatulia na kuendelea na mambo
yake bila kujali kuwa anafanyiwa ukatili wa kijinsia.
Bi. Faidha Twalib akichangia mada kwenye semina leo jijini Dar es salaam |
Na tatizo la ubakaji lipo kwa asilimia ndogo sana katika
maeneo hayo na imeelezwa kuwa mambo hayo
utekelezwa usiku kwa wale mabinti wanaopenda vigodoro na kushindwa
kutulia makwao mpaka usiku wa manane wanazunguka kufuata miziki huwa ndio
wanapata madhara hayo kwa kuwa kwenye shughuli hizo wanakuwepo watu toka maeneo
tofauti tofauti siyo Mburahati peke yake.
Bw. Abdalaah Salehe akitoa maoni yake kwenye semina mapema leo jijini Dar es salaam |
Mwisho kabsa walipenda kutoa ushauri kwa serikali kuweza
kuwarudisha shuleni wanafunzi wanaopata ujauzito waweze kurudi baada ya
kujifungua kwa kuwa hawatafanya mchezo kutokana watakuwa wamejifunza vya kutosha kwa
waliyoyapitia. Hivyo haitakuwa na maana kuwaacha tena mtaani kwani hali hii
itawapa mwanya wazazi wa kuwaozesha ingawa umri wao ni mdogo.
Na pia walipenda kuwaelimisha wazazi wenzao wa kata ya Mburahati kujenga tabia ya kukaa chini na kuongea na watoto wao ili
kuwafundisha maadili mema na kuwapa elimu ya uzazi ili kukabiliana na changamoto wanazokutana
nazo na jinsi ya kizitatua.
baadhi ya wageni warioudhuria semina hiyo |
Pia waliomba kwa TGNP mtandao kuwa na mawakala au vikundi
mbalimbali kwenye kila kata ili kuweza kusambaza elimu hii zaidi na watu
mbalimbali waweze kupata elimu ili wawaondokane na ukatili huu unaoendelea kwa
sasa.
No comments:
Post a Comment