Siku chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutangaza kujitosa kwenye mgogoro wa Chama cha Wananchi CUF, Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya ameibuka na kusema hawatazivumilia hujuma za chama hicho.
Naibu katibu mkuu wa CUF Magdalena H. Sakaya akiongea na waandishi wa habari mapema jana makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam |
Akizungumza katika Ofisi za CUF Makao Makuu Buguruni, Sakaya amesema mara kadhaa wameripoti matamko ya viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiingilia mgogoro wa CUF.
“Chadema wamekuwa na vikao kadhaa na mkakati wa kuhakikisha wanaifuta CUF upande wa Bara, miongoni kwa mipango hiyo ni kuvamia Ofisi pamoja na kuratibu na kukusanya vijana wa kihuni.” – Magdalena Sakaya.
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria mkutano huo mapema jana jijini Dar es salaam |
Aidha, Sakaya amesema kuwa CUF wanalichukilia jambo hilo kuwa ni kushindwa kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamadi kuiuza CUF kwa Chadema.
“Tunawataka Watanzanua wafahamu kuwa CUF ni chama kilichosajiliwa kwa mujibu wa sheria na kina Katiba yake. Hivyo hatutotoa fursa ya kufanyiwa maamuzi nje ya vikao vya chama na tunatoa onyo kwa viongozi wa CHADEMA.” – Mgdalena Sakaya
Baadhi ya wanachama wa CUF wakiimba nyimbo za kujigamba kuonyesha kutowaogopa CHADEMA. |
No comments:
Post a Comment