BEKI Vincent Bossou, rasmi ameshindwana na Yanga lakini amepata neema baada ya kuitwa katika kikosi cha timu ya Bidvest Wits ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Bossou, raia wa Togo, ambaye aliichezea Yanga kwa mafanikio na kuisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, baada ya kumaliza mkataba Jangwani hivi karibuni, amewachenjia viongozi wa timu hiyo akitaka dau kubwa ambalo wameshindwa kumpa na kuamua kuachana naye.
Kwa mujibu wa barua rasmi ambayo Championi Jumatano limeinasa ambayo iliandikwa na wakala wake Gibby Kalule kwenda kwa Yanga, beki huyo alitaka dau la usajili la dola 42,000 ambayo ni sawa na Sh milioni 92, mshahara wa dola 4,200 (Sh milioni 9.2) kila mwezi, tiketi mbili za ndege kila mwaka kwa ajili ya yeye na mkewe wakati wa mapumziko pamoja na bonasi ya dola 5,000 (Sh milioni 11) kama timu hiyo itatwaa ubingwa.
Kwa dau hilo, Yanga hawakuwa tayari kulitoa, hivyo kujibu barua kwa wakala huyo kwamba haitawezekana na wanamtakia kila la kheri. Barua hiyo pia tunayo. Hata hivyo, juzi Jumatatu, Bidvest ilimuandikia barua wakala huyo, ikieleza kuwa
No comments:
Post a Comment