Cuf-Chama Wananchi
Kimewaita Wabunge wake 10 na Madiwani wake 2 Viti Maalum wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kutokana na sintofahamu iliopo ndani ya Cuf. Kamati ya Nidhamu na Maadili imekusudia kuwaita wale wote waliohusika kwa namna moja au nyengine katika mgogoro unaondelea ndani ya Chama. Watuhumiwa hao wataitwa kwa Makundi kama ifuatavyo
1. Kundi la Wabunge na Madiwani Viti Maalum
2 . Kundi la Wabunge na Madiwani wa Majimbo na Kata
3 . Viongozi wa Chama ngazi ya Wilaya
Kesho Jumapili Tarehe 23/07/2017 wafuatao wanahitajika mbele ya Kikao cha Kamati ya Nidhamu na Madili kitachofanyika Ofisi Kuu za Cuf Buguruni ukumbi wa Shaban Khamis Mloo saa 3:00 asubuhi .
1. Riziki Shahali Ngwali
2 .Saverina Mwijage
3 .Salma Mwassa
4 .Saumu Sakala
5 .Riziki Lulida
6 .Mgeni Jadi Kadika
7 .Raisa Abdallah Mussa
8 .Miza Bakari
9 .Halima Ali Mohammed
10 Khadija Al Kassim
11 Leila Hussein Madibi Diwani Viti Maalum Ubungo
12 Elizabeth Magwaja Diwani Viti Maalum Temeke
Wanachama hao watahojiwa mbele ya Kamati ya Maadili na kisha kufikishwa mbele ya Kikao cha Baraza Kuu siku hiyo hiyo saa 8:00 Mchana katika ukumbi huo huo wa Shaban Khamis Mloo.
Baada ya kukamilika kwa Mahojiano ya kundi la kwanza, itafuatiwa na makundi mengine katika muda utaopangwa
Mpaka sasa waliotajwa hapo juu, wamwshajulishwa kuhusu Kikao hicho, kwa hivyo Kikao kitafanyika kama kilivyopangwa.
HAKI SAWA KWA WOTE
Masoud Omari Mhina
Naibu Katibu wa Kamati ya Nidhamu na Maadili
No comments:
Post a Comment