Tuesday, July 11, 2017

WAHENGA NI WAKINA NANI-MAANA HALISI HII HAPA

Katika Mitandao ya kitanzania kwa Takribani wiki moja sasa kumekuwa na Utani unaofurahisha sana kuhusu matumizi ya neno wahenga,Wengi Tumekuwa tukilitumia neno hili tangu zamani ambapo kwa Sasa Pia Limeanza kushika kasi japo kwa mfumo Mwingine wa mzaha mwingi,Nimeona ni vyema nikashea na wewe kidogo maana ya neno wahenga ili tuweze kupata ufahamu kidogo,soma Hii

Wahenga ni 'ancestors'. Unajua zamani kabla ya development of technology watu walikuwa wanajifunza mambo mbalimbali ya maisha kuanzia afya, ulinzi etc kutokana na matukio yanayowakuta. Mfano mama mjizo anapokula sana aina fulani ya chakula na matokeo yake kufanya mtoto kuwa mkubwa kiasi kwamba njia ya kawaida ya kujifungua ilikuwa haiwezekani na hivyo kupoteza maisha, basi wazee walikuwa wanakusanya matukio kama haya na kuangalia sababu wakigundua wanakaa chini na kuona jinsi ya kuzuia matukio hayo kwa kutumia taarifa tu. Unakuta wanaanzisha misemo kama 'Mama mjamzito akila mayai, mtoto atazaliwa bila nywele' - ujumbe huu ulikuwa na nguvu sana katika kuzuia excessive eating of eggs kwa wajawazito.


Misemo mingi ilikuwa ikiwekwa na wazee kwa ajili ya kuzuia matukio mabaya waliyokumbana nao katika jamii. Wazee hawa walikuwa wanaaminika sana na jamii. Hivyo basi vizazi vijavyo navyo vinachukua maneno hayo na kuyaendeleza indirectly wanakuwa wanajikinga na majanga ambayo wazee waliisha yafanyia obervation research. 

Mfano tu ni 'Bahati ya mwenzako usiilalie mlango wazi' - ina maana kubwa sana, kama mtu ameepuka janga fulani basi usidhani kuwa ni guaranteed, ndiyo maana katika ajali kuna wanaopoteza maisha na kupona, kwenye ukimwi kuna wanaosahau kutumia co'ndom na kujikuta hawajaambukizwa kwa hiyo usichukukulie kuwa ni kawaida kutokea hivyo, Inawezekana methali hii ,enzi za mababu ikawa ilitokana na 'mwanajamii kusahahu kufunga mlango na usiku swala akaingia ndani na kujipatia kitoweo, ila wakati huohuo kuna mwingine alisahau akaingiliwa na simba na kuliwa'. Haya yote yalitokana na Observation za wazee hao waliokuwa wakiishi enzi hizo.

No comments: