Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Kwinga, akizungumza na maofisa Ugani wa wilaya hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani kutoka kata zote na vijiji vya wilaya hiyo wilayani humo leo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Martha Susu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Adam Malunkwi.
Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Margareth Nakainga, akizungumza katika mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Adam Malunkwi, akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa wilaya hiyo kufungua mafunzo hayo. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Paschal Byemelwa.
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange akitoa mada.
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wa wilaya hiyo, Abdulusalam Kajuna, akizungumza.
Mtafiti wa zao la Pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ugirigulu Mwanza, Stellah Chilimi akitoa mada.
Maofisa ugani wakiwa katika mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Semina hiyo
Maofisa ugani wa wilaya hiyo wakijitambulisha kwa mkuu wa wilaya.
Wanahabari wakiandaa taarifa hiyo. Kulia ni Doreen Mlay wa TBC na Hellen wa Time FM.
Picha ya pamoja ya maofisa ugani na mgeni rasmi mkuu wa wilaya.
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora, Angelina Kwingwa ameomba watafiti nchini kufanya utafiti wa mazao ya chakula yanayostahimili ukame ili kuwezesha wananchi
Ombi hilo amelitoa leo wakati akifungua mafunzo kwa maafisa ugani wote wa wilaya hiyo yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia( COSTECH), kupitia Jukwaa
la Bioteknojia kwa maendeleo ya kilimo (OFAB) yenye lengo la kuwawezesha maofisa ugani kutumia teknolojia na tafiti katika kupunguza changamoto zinazowakabili
wakulima na kuongeza tija.
Amesema wananchi wa wilaya hiyo zao lao kuu ni Tumbaku ambalo nilo zao la biashara lakini wanategemea sana Mahindi pamoja na mpunga ingawa mabadiriko ya tabia ya
nchi yamekuwa yakiathiri sana uzalishaji wa mazao hayo ya chakula na kupelekea baadhi yao kuwa na upungufu wa chakula.
“Watafiti tunaomba mtuletee mbegu bora za mihogo ambazo zinakinzana na magonjwa ya batobato na michirizi ya kahawia kama zamamani kwani mihogo ya wakulima ya asili ambayo ilikuwa mizuri na iliyowapa tija wakulima miaka ya nyuma imepotea kutokana na kushambuliwa na magonjwa” alisema Kwingwa.
Ameishurkuru COSTECH kwa kupeleka mafunzo hayo kwenye wilaya yake ili kuwakumbusha wataalamu hao wa ugani mbinu bora za mazao ya mihogo,mahindi,mpunga na viazi lishe
ambayo ni mazao muhimu kwa chaula kwa wakazi wa wilaya na zao la biashara la pamba kama ambalo litasaidia na zao la Tumbaku katika kuongeza uchumi kwenye kaya.
Ameahidi msimu ujao kutembea kila kata kuangalia kama wakulima wamepelekea mbinu hizo walizofundishwa kwa kukagua mashamba na kuwauliza maswali ili kuhakikisha
kuwa mafunzo hayo yanaleta tija iliyokusudiwa ikizingatiwa kuwa Rais Dk.John Magufuli alishasema hataki kusikia njaa wilaya yoyote.
“Hakuna uchumi wa kati na viwanda endapo wakulima hawataweza kuzalisha mazao na malighafi za kutosha kulisha viwanda ambavyo serikali ya awamu ya tano
inavihamasisha kujengwa na wataalamu hawa ndio watakaowezesha wakulima kuzalisha malighafi hizo za kutosha sipo tayari kuonekana siendani na kasi ” alisisitiza
Kwingwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo ya Urambo Magreth Nakainga amesema wakulima wengi hivi sasa wanaotegemea zao la Tumbaku hawana hela na wanashindwa kumudu kujikumu kwenye mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kutokana na wanunuzi wa zao la Tumbaku kutofika kununua tumbaku ya wakulima kwa wakati.
Amesema wakulima wamelima vizuri na kuzalisha Tumbaku ya kutosha lakini wamebaki na Tumbaku yao majumbani mwao hali ambayo inawadhoofisha kimaisha kutokana na
fedha walizozitegemea kwenye kupeleka watoto shule,kununua mahitaji mengine hazijanunuliwa na wanunuzi wa tumbaku na hivyo kukwamisha maendeleo ya wakulima.
“ Hivi sasa tunahimiza zao la Pamba kwa wakulima wetu kwenye wilaya nzima kutokana na soko la Tumbaku kutokuaminika husussani soko lake kwahiyo mafunzo haya
yatasaidia sana kuamsha maafisa ugani wetu kupata dozi ya kutosha kuwafundisha wakulima kukimbilia zao la Pamba” alisema Nakainga.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Adam Malunkwi amesema halamashauri hiyo itahakikisha mafunzo hayo yanatekelezwa kwa vitendo kwenye mashamba ya wakulima kwakuwa wamewawezesha kila afisa ugani kupata baiskeli katika awamu ya kwanza lakini pia sasa wamewapatia pikipiki maafisa ugani wote ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Amesema umefika wakati sasa wakulima wapewe mbegu bora za mpunga ambazo zinastahimili ukame kutokana na hasara kubwa waliyoipata wakulima msimu uliopita ambapo pamoja na kulima vizuri lakini mpunga wao umekauka na hivyo kuwakosesha
chakula wakulima wengi ambao wanalima kwenye mabonde.
Katika hatua nyingine amelalamikia baaadhi ya mbegu za kilimo wanazouziwa wakulima hazioti na hazifanyi vizuri kwenye wilaya hiyo na hivyo kuomba watafiti na wauzaji
wa mbegu kuwapelekea wakulima mbegu ambazo zinastahili kulimwa kwenye udongo wao.
"Watafiti na serikali mtusaidie kufanya uchunguzi wa mbegu hizi zinazoletwa kwa wakulima wetu maana wanazinunua dukani na zina nembo zote ila hazioti na zikiota
hazifanyi vizuri" alisema Makwinkwi.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
No comments:
Post a Comment