Friday, July 14, 2017

WAZIRI KAIRUKI - WATUMISHI WA UMMA WANATAKIWA KIJISAJILI KWENYE MFUMO UTAKAO TUNZA TAARIFA ZAO

Watumishi wa Umma wametakiwa kujisajili kwenye mfumo utakao wawezesha kujua taarifa zao mbalimbali lakini pia utakao wapa nafasi ya kutoa maoni yao na changamoto mbalimbali zinazopatikana maeneo yao ya kazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umaa Angel Kairuki akiongea na watumishi wa Umma mambo mbalimbali mapema leo jijini Dar es salaam ikiwa ni wiki ya Utumishi wa Umma 
 Akiongea kwenye mkutano huo waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umaa Angel Kairuki alisema kuwa ni vema kwa watumishi wa umma kujisajili kwani mfumo huu utachukua taarifa binafsi na kulinganisha na taarifa za Nida ili kuweza kupata uhakika kwani hii itafanya haki kutendeka kwa wote kwa kuwa kuna watumishi wamepandishwa vyeo zaidi ya mara tatu lakini taarifa zinaonyesha mara moja au mbili.
Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Bw. Aron Kagurumjuli akitoa mchango wake kwenye maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma wilaya ya Kinondoni mapema leo jijini Dar es salaam
Tovuti hiyo mahususi kwa watumishi wa Umma ambayo ni www.watumishiphoto.utumishi.co.tz  Bi. Angela Kairuki alisema ifikapo tarehe 7 januari kila mtumishi anatakiwa kuwa amejisajiri ili afahamike na taarifa zake ziwepo kuepuka tatizo la kuajiri watumishi wasio na sifa na tatizo la kulipa watumishi wenye malimbikizi mara mbili au kuwalipa zaidi.
Baadhi ya watumishi wa Umma wakifuatilia semina iliyoendeshwa mapema leo jijini Dar es salaam
Faida nyingine watakayoipata watumishi wa Umma ni kuweza kujua taarifa za mishahara yao na makato yao wanayokatwa kwa kila mwezi, lakini pia inawasaidia pale wanapohitaji kwenda kukopa benki kuweza kuonekana kwa taarifa zao kwenye mfumo huo ivyo kuwapa urahisi wa kupata mikopo.
Baadhi ya watumishi wa umma wakifuatilia semina mapema leo jijini Dar es salaam
Na kwa wafanyakazi kama walimu inawapa nafasi ya kuweza kubadilishana vituo vya kazi kwa kuangali nani anasifa zinazofanana na zako ukiona unapeleka taarifa kwa mkurugenzi na mnaweza kubadilishana tofauti na hapo mwanzo tangazo linawekwa kwenye ubao(notes board) hali inayoweka ugumu kupata taarifa kwa urahisi.

Lakini pia alisema kuwa serikali ipo kwa ajili ya wananchi na kila mtu atapata haki yake kwa wale waliopandishwa vyeo basi watapewa vyeo vyao na kwa wale wenye malimbikizi ya mishahara kwa msimu huu wa 2017/18 watalipwa madeni yao yote.


Na kwa upande wa ajira alisema kuwa ajira zaidi ya 10180 zitatolewa hii ikiwa ni kuziba mapengo ya watumishi hewa na ambao hawakuwa na vigezo na ajira mpya zitatolewa zaidi ya 52436 kwa idara mbalimbali za serikali.

No comments: