Kundi la muziki wa hip hop Bongo, Weusi wamesema ujumbe uliokusudiwa katika ngoma yao mpya ‘Amsha Dude’ umefika.
Rapper Joh Makini amesema ishara ya wimbo huu kufika ni pale watu wanapokuwa na tafsiri tofauti tofauti katika mstari mmoja kitu kinachoashiria mstari husika ni mkubwa.
“Mtu mwingine anaweza kuutumia kwa matumizi yake mengine, na wewe unaweza kuutumia kwa matumizi yako mengine lakini the same time wote mnapata burudani na target yetu kubwa ni kuhakikisha muziki unakuwa mkubwa,” Joh Makini ameiambia Planet Bongo ya EA Radio.
Kwa upande wake Nikki wa Pili amesema, “ujumbe ni kwamba amsha dude katika lolote unalolifanya, kama unatangaza usikwepeshe, amsha dude, kama unafanya mixing, amsha dude, na kama una ndoa amsha dude”.
No comments:
Post a Comment