Friday, August 18, 2017

AFYA-USICHOKIFAHAMU KUHUSU INI LAKO

                                                                  
 AFYA YA INI
Kuna vitu vya pekee sana katika mwili wako kama vile ini: Siyo kwamba ini  ni kiungo kikuu tu katika mwili wa mwanadamu lakini pia lina fanya kazi nyingi kuliko viungo vingine vingi katika mwili. Kuchuja sumu mwilini, hutoa nyongo inayosaga chakula, kuongoza kemikali mbalimbali mwilini. Uharibufu wowote ukitokea katika ini hakuna awezaye tena kufanya marekebisho ili ini liweze kuendelea na kazi yake. Ini hakika ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu.
 
KUNA MAMBO MAKUU SITA YANAYOPELEKEA UHARIBIFU WA INI
1.      Kulala kwa kuchelewa sana na kuchelewa kuamka asubuhi.
a.       Saa 3-5 Usiku ni mda ambao mwili unajisafisha kuondoa sumu na madawa (detoxification) katika mwili (lymph nodes) muda huu mtu anapaswa kupumzika au kusikiliza muziki wa taratibu kwaya isiyokuwa na midundo. Kama mda huu mama atakua akihangaika na watoto mara vyombo basi hatua hii ya kuondoa sumu haitafanyika vizuri na haitakua na matokeo chanya.
b.      Saa 5-7 Usiku Sumu inakua ikiondolewa katika Ini. Inafanyika mtu anapokuwa katika usingizi mzito
c.       Saa 7-9 Usiku Uondoaji wa sumu unahamia kwenye gall bladder pia hufanyika wakati mtu akiwa katika usingizi mzito
d.      Saa 9-11 Asubuhi Sumu inaondolewa katika mapafu, hivyo mtu anaweza kukohoa au chafya, mtu haitaji kutumia dawa kwasababu uondoaji wa sumu umefika katika mfumo wa hewa.
e.       Saa 11-1 Asubuhi Sumu inaondolewa katika Colon utumbo unakuwa hauna kitu.
f.       Saa 1-3 Asubuhi mwili unanyonya virutubisho kutoka utumbo mdogo. Hakikisha unapata kifungua kinywa cha maana kwaanzia 1230-3000Asubuhi. Kuchelewa kulala na kuchelewa kuamka inaharibu mpangilio wa uondoaji sumu hivyo Ini linajawa na sumu.
2.      Kutokukojoa asubuhi na Kutopata kifungua kinywa
3.      Kutumia dawa nyingi za hospitalini marakwamara (Drugs)
4.      Kula kupita kiasi {overeating} hii ni njia kuu ya kufanya uharibifu katika ini lako, wewe kula tu kila kitu unachotamani na utavuna uharibifu wa ini.
5.      Kula na kunywa visivyofaa: kuna baadhi ya vitu ambavyo ini lako halipendi hata kukutana navyo mfano ngano nyeupe, vyakula vya viwandani kama vile juisi na vyakula vyote vitengenezwavyo viwandani{prossesing food, refined white flour product} na baadhi ya mafuta.
6.      Kukosa  vyakula vyenye protein pamoja na fati.
7.      Kula vyakula vibaya kama vile caffeine, alcohol {pombe kwa aina zake zote}  na madawa ya kulevya.
8.      Kuvuta hewa yenye sumu huathiri ini moja kwa moja.
Note: jitahidi kuupenda mwili wako kwa kula vyakula na vinywaji vyenye kuujenga mwili wako kwa kuwa utapata afya njema kumbuka Mungu amekupatia hekalu lake ili kulitunza kwa kula vizuri kwa afya kushindwa kuutunza mwili wako kwa uzembe ipo siku utadaiwa na yule aliyekupatia.
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na bbc umebaini kuwa, Homa ya Ini husababishwa na Ngono isiyosalama ambapo Mwanaume na Mwanamke hulambana sehemu za siri. Ni vyema kushiriki tendo la ndoa kwa mwenzi mmoja na usafi uwe kipaumbele.
                               NAMNA YA KUTUNZA INI LAKO
·         Hakikisha unakula vyakula vyenye potassium kwa wingi kama vile mchele, ndizi, ngano nyeusi, mbegu mbalimbali kama vile mbegu za maboga, mbegu za matunda mbalimbali, almond na vingine vingi vinavyofanana na hivyo.
·         Kunywa maji kwa wingi. Kunywa kidogo kila bada ya muda. Mfano asubuhi unapoamka kunywa glass mbili za maji, baada ya masaa mawili kunya glass moja kunywa baada saa moja. Hakikisha kila unapoenda kuoga unakunywa maji glass moja, wakati unapoenda kulala kunywa glass moja ya maji.
·         Kunywa juisi ya matunda kwa wingi, tengeneza juisi mwenyewe hasa juisi ya carrot na beet.
·         Jitaidi kutumia mafuta kidogo kwa chakula na jitaidi kutumia alizeti kuwa sehemu kubwa katika matumizi ya vyakula vyako.
·         Jitaidi kula matunda ya apples kwa wingi angalau kila siku apple moja.
·         Tangawizi ni nzuri kwani ina nafasi kubwa ya kulinda ini lako, fanya tangawizi kuwa sehemu ya kinywaji chako kila siku.
                                 TUMAINI
Ni wale tu wanaosoma neno la Mungu  na kusikia  sauti ya Mungu  ikisema nao ndio wanafunzi wa kweli. Wanatetemeka wanaposoma neno la Mungu kwa hao ndio wanaoishi ukweli, na ili kuisikia sauti ya Mungu tunapaswa kumsihi Mungu  atuwezeshe na kumkabidhi yeye yale yote yanayotutenganisha na yeye.
 
Ubarikiwe sana Rafiki!! Baada ya kusoma mafundisho haya, Je sasa unaamini kwa usahihi hali ya Wafu? Je ungependa kujifunza Zaidi?. Tafadhali tuandikie tujifunze2017@yahoo.com kwa swali au namna ya kuboresha huduma zetu. Pia kama kuna mada inakutatitiza usiache kutuandikia.

No comments: