Benki ya KCB ikifanya
ziara katika kituo cha Montessori School and Orphanage.
|
Uongozi na wafanyakazi wa
Benki ya KCB kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori School and Orphanage Bi.
Susana H. Maziku (waliokaa, watatu kushoto) na watoto wa kituo hicho.
|
Baadhi ya
watoto wa Montessori School and Orphanage wakitoa burudani kwa uongozi wa benki
ya KCB.
|
Benki
ya KCB Tanzania imekabidhi misaada mbalimbali kwa kituo cha watoto yatima
Montessori School Orphans Organization kisiwani Unguja.
Akizungumza wakati wa hafla
ya makabidhiano, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Bw, Cosmas Kimario alisema kuwa mchango huo upo ndani
ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii
zilizo na uhitaji.
“Benki ya KCB Tanzania inadhamini
uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya
vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni
kujikita katika masuala ya ubinadamu”, Bw. Kimario alisema na kubainisha kwamba
tangu benki hiyo ilipofunguliwa hapa Tanzania mwaka 1997, benki hiyo imekuwa
ikijikita katika kuisadia jamii.
Alisema ni vyema jamii
ikatambua uwepo wa watoto waishio katika mazingira magumu na wale walioko
kwenye vituo, kwa kuwapatia mahitaji mabalimbali kama wanavyopata watoto wa
majumbani kwani ni haki yao ya msingi. “Tukiwajali hawa watoto hata kwa Mungu
tunapata dhawabu kwani wengi wao hawajapenda kuwa katika mazingira haya”
alisema Kimario.
Bw.
Kimario, Alielezea kuhusiana na programu endelevu inayoitwa KCB 2jiajiri, na
kusema; “KCB 2jiajiri ni programu inayowapa elimu ya nadharia na vitendo
wanawake wajasiriamali nchini. Zanzibar, KCB 2jiajiri imefundisha wanawake 32
darasani na maafisa wetu watatu ambao ni wa masoko, fedha na sheria
wanazitembelea biashara za wakinamama hao ili kuwapa elimu kwa vitendo.”
Benki ya KCB ilikabidhi
misaada mbalimbali ikiwemo magodoro, mashuka, neti na vyakula.vyenye thamani ya
shilling 2,963,000. Mwenyekiti wa bodi ya KCB Bi. Zuhura Sinare Muro alielezea
kuhusiana na mchango wa benki hiyo Zanzibar na kusema “Benki ya KCB mbali na
kufanya biashara imekuwa ikijihusisha katika miradi mbalimbali yenye manufaa
kwa wazanzibari wahitaji.”
Bi. Muro alizitaja baadhi ya
michango iliyotolewa na benki hiyo ili kuinua hali ya maisha ya wananchi wenye
shida kuwa ni; ujenzi wa kisima
cha maji Mazizini Orphanage Centre, utoaji wa vyakula mbalimbali kwa Zanzibar
Hayunani Association, vifaa vya kusomea na kuandikia katika shule ya Bwefum na
vifaa tiba katika hospitali za Kivunge
Cottage, Mwembeladu na Kombeni. Kwa misaada hii yote Benki imetumia zaidi ya
milioni 100.
Mkurugenzi wa kituo cha
Montessori School Orphans Organization Susan H. Maziku aliishukuru benki ya KCB
kwa mchango wake katika kituo hicho na kuwataka makampuni na jamii kuiga mfano
huo wa kuwakumbuka watoto yatima wenye uhitaji mkubwa sana.
No comments:
Post a Comment