Degedege ni hali ya ghafla ya kutingishika mwili mzima au mikono na miguu kunako sababishwa na kukakamaa kwa misuli ya mwili.
Homa ni Nini?
Ni hali ya kawaida ya mwili kujikinga na maambukizi. Na kwa watoto hutokea pale joto la mwili linapokuwa zaidi ya nyuzi 38 za sentigredi.
Homa ya Degedege Ni Nini?
Ni degedege linalotokea kwa watoto ghafla likiambatana na homa kali iliyotokana na kuongezeka haraka kwa joto la mwili. Ugonjwa huu utokea kwa wastani wa asilimia nne (4%) ya watoto walio kati ya umri wa miezi sita na miaka mitano. Watoto wengi ambao hupatwa na ugonjwa huu huwa haiwapelekei baadae kuwa na matatizo ya kudumu kama kupata ugonjwa wa kifafa, ni asilimia tatu (3%) tu ambao wanaweza baadae kupata ugonjwa wa kifafa.
Mmoja kati ya watoto watatu ambao wamewahi kuwa na homa ya degedege wanaweza wakapatwa tena na tatizo hili.baadhi ya watoto wanaweza wasipatwe kabisa na tatizo hili au wakapatwa mara moja tu kwa maisha yao yote. Lakini hauna jinsi ya kutabiri ni mtoto yupi ambaye anaweza kupatwa na shambulio hili.
Homa ya Degedege Hutokea kwa Watoto Gani?
Watoto wanaweza kurithi tabia hii ya kuumwa homa ya degedege kutoka kwa wazazi wao. Kama mama au baba aliwahi kuumwa ugonjwa huu basi mtoto ana asilimia 10-20 zaidi ya kuumwa ugonjwa huu hukilinganisha na yule ambaye wazazi wake hawakuwai kuumwa ugonjwa huu.
Homa inasababishwayo na maabukizi yoyote yale kama virus, bakteria na parasite
SABABU
Tatizo la degedege mara nyingi linatokana na magonjwa au hitilafu katika ubongo.
Na kwa kawaida hali ya degedege haitokei moja kwa moja kwa mtu inakuja na kuachia baadhi ya watu wanaamini dawa zao walizofanya ndiyo imemuachia wakati dege dege inaweza kuacha kuendelea hata bila dawa.
DALILI:
Shambulio la ugonjwa huu likijitokeza uanza na kupotewa na fahamu na muda mfupi baadae mwili, miguu na mikono uanza kukakamaa na kurudisha kichwa nyuma, baada ya hayo miguu na mikono uanza kujitikisa.
KINA NANI HUWAPATA ZAIDI DEGEDGE?
Degedege inaweza kumpata mtu yoyote wa umri wowote ijapokuwa mara nyingi inawatokea watoto wadogo walio na umri chini ya miaka mitano.Ndio maana wengine wanaita homa ya watoto/kitoto
NINI CHA KUFANYA MTU AKIPATWA NA DEGEDEGE?
Mgonjwa mwenye degedege asipopata tiba sahihi kwa wakati anaweza kupatwa na madhara yafuatayo

- Magonjwa ya ubongo kama Kifafa.
- Upungufu wa vichocheo kwenye damu kama upungufu wa sukari kwenye damu (Hypoglycemia) na upungufu wa hewa ya Oksjeni ya kutosha kwenye damu(Hypoxia).Kwa kuwa vitu hivi vipo katika kiwango kidogo kwenye damu hali hii itapelekea ubongo nao usiwe na sukari na Oksjeni ya kutosha hivyo kutofanya kazi yake sawa sawa.
- Kuwa na shinikizo la chini la damu.
- Kuwa na maambukizi mwili kama yatokanayo na vimelea vya bacteria (SEPCEMIA),au Fangasi (Cryptococcal),Virusi hasa HIV wanapoingia kwenye ubongo.
- Kuwa na homa kali itokanayo na Malaria au Uti wa mgongo(Meningitis).
Na kwa kawaida hali ya degedege haitokei moja kwa moja kwa mtu inakuja na kuachia baadhi ya watu wanaamini dawa zao walizofanya ndiyo imemuachia wakati dege dege inaweza kuacha kuendelea hata bila dawa.
DALILI:
Shambulio la ugonjwa huu likijitokeza uanza na kupotewa na fahamu na muda mfupi baadae mwili, miguu na mikono uanza kukakamaa na kurudisha kichwa nyuma, baada ya hayo miguu na mikono uanza kujitikisa.
- Kushindwa kupumua na kutokwa na mapovu mdomoni
- Macho kugeukia nyuma na kuonekana kwa sehemu nyeupe ya jicho
- Shambulio huisha baada ya muda mfupi mara nyingi chini ya dakika tano
- Baada ya shambulio hupitiwa na usingizi mzito kama takribani dakika 30 hadi saa nzima.
- Akizinduka anaweza kushindwa hata kukutambua na akawa atamani kitu chochote kwa muda huo.
KINA NANI HUWAPATA ZAIDI DEGEDGE?
Degedege inaweza kumpata mtu yoyote wa umri wowote ijapokuwa mara nyingi inawatokea watoto wadogo walio na umri chini ya miaka mitano.Ndio maana wengine wanaita homa ya watoto/kitoto
NINI CHA KUFANYA MTU AKIPATWA NA DEGEDEGE?
- Msaidie mgonjwa alale upande.
- Ondoa vitu vyovyote (vigumu au vyenye ncha kali) vinavyoweza kumdhuru mgonjwa.
- Weka kitu laini mfano nguo iliyokunjwa chini ya kichwa cha mgonjwa.
- Usimpulizie hewa mdomoni; fanya hivyo iwapo hataweza kupumua baada ya degedege kukoma.
- Fungua nguo au kitu chochote kilichoko kwenye shingo ambacho kinaweza kuathiri upumuaji.
- Usijaribu kumzuia mgonjwa kwa kumkandamiza au kushika mikono na miguu
- Kuwa mtulivu na hakikisha wale wote waliowazunguka wanakuwa watulivu.
- Baki na mgonjwa hadi degedege litakapokoma lenyewe
- Onesha upendo wakati anaporudiwa na fahamu
- Iwapo ataonekana kuchanganyiwa, omba msaada.
Mgonjwa mwenye degedege asipopata tiba sahihi kwa wakati anaweza kupatwa na madhara yafuatayo
- Kupata tatizo la Kifafa.
- Mtindio wa ubongo kwa watoto inaweza kupelekea ulewa duni katika masomo na hata mambo mengi akiwa nyumbani.
- Ukuaji duni kwa mtoto hasa kama degedege ikiwa itamtokea mara kwa mara na hatimye motto atadumaa.
- Kuwa na usikivu duni na uoni hafifu.
- CHANZO MUUNGWANA BLOG
No comments:
Post a Comment