Saturday, August 12, 2017

Jiji la Dar es Salaam lanunua gari ya kubebea Marehemu wasio kuwa na ndugu, Meya Mwita atoa neno.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari jana mara Baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa gari la kubebea Marehemu wasiokuwa na ndugu.

Muonekano wa nje wa gari la kubebea Marehemu wasiokuwa na ndugu.

Muonekano wa ndani wa gari la kubebea Marehemu wasio kuwa na ndugu katika Jiji la Dar es Salaam.
Picha zote na Christina Mwagala , Ofisi ya Meya wa Jiji.

  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwaonyesha waandishi wa habari na watendaji wa Halmashauri ya jiji gari lililonunuliwa kwa ajili ya kusafirisha Marehemu wasiokuwa na ndugu.

NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
HALMASHAURI ya jijj la Dar es Salaam limenunua gari la kubebea marehemu wasio kuwa na ndugu na kuzinduliwa jana na Mstahiki Meya wa Jiji Isaya Mwita .
Gari hilo litatumika kubebea miili ya marehemu waliokuwa hawana ndugu jijini hapana na hivyo kupelekwa kwenye makaburi kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua gari hilo, Meya Mwita alisema kuwa jiji limefikia hatua hiyo ili kuondoa usumbufu wanaopata watu pindi wanapopoteza maisha hivyo hivi sasa watapata huduma ya usafiri kama ilivyo kwa wengine.
Aliongeza kuwa gari hilo litatoa huduma kwa kila mwananchi ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam bila kujali itikadi ya vyama, dini, kabila kwa kuwa wote ni Watanzania .
" Tumeona kwamba wenzetu ambao hawana ndugu katika Jiji letu wanapo poteza maisha huwa wanapata tabu kutokana na kukosa huduma hii , lakini kama Jiji sasa tumenunua hili gari ambalo litatumika kuwasafirisha kwenda kuhifadhiwa kwenye makaburi yaliyopo ijiji hapa.
Aidha pesa ambazo zimetumika kununulia zimetokana kwenye bajeti ya mwaka wa Fedha wa 2016/ 2017, gari hili nikubwa linauwezo wa kuchukua watu wa nne, nitoe wito kwa wakazi wa jiji letu kwamba gari lipo ule usumbufu sasa hautakuwepo"alisema Meya Mwita.

No comments: