leo ikiwa tarehe 4 agost Mahakama kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelitupilia mbali ombi la wabunge 8 wa CUF waliokuwa wakipinga kuapishwa wabunge wapya walioteuliwa na chama hicho.
Wakili wa bodi ya wadhamini ya chama cha wananchi CUF Bw. Mashaka Ngole Akiongea na waandishi wa habari mapema leo nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es salaam |
akiongea nje ya ukumbi wa mahakama wakili wa bodi ya wadhamini ya chama cha wananchi CUF Bw. Mashaka Ngole alisema kutokana na kuwepo kwa mapungufu kwenye mashauri yaliyowasilishwa na upande wa madai na hivyo Mahakama kutupilia mbali shitaka hilo.
"lakini pia kama upande wa madai wataona hawakuridhishwa na hilo basi wanaruhusiwa kuleta tena maombi Mahakamani na kwa sasa hakuna kinachozuia wabunge wateule wasiapishwe, na kinachosubiriwa ni bunge kuweza kutimiza wajibu wake kwani pingamizi limeshatolewa". alisema Mashaka
Baaddhi ya wanachama wa CUF wakisubiri mashitaka kuanza kusomwa |
Na mwisho alisema endapo watashindwa kuleta maombi ya kuweka pingamizi basi itabidi walipe fidia kwa kuwasumbua na kuleta mahakamani hoja zisizo na msingi hivyo bado hawajaamua kiwango cha kulipwa endapo watashinda kesi.
No comments:
Post a Comment