Thursday, August 3, 2017

Maamuzi ya mahakama kesi ya Seth na Rugemalila

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kesi inayowakabili mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL , Harbinder  Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemalira wanaokabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia serikali hasara.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 17, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na kumpa siku 14 Sethi aweze kutibiwa hapa nchini tofauti na wakili wake, Alex Balomi aliyetaka mteja wake huyo apewe ruhusa na mahakama hiyo ili kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Awali, mawakili wanaomtetea mfanyabiashara Sethi waliiomba Mahakama imruhusu mteja wao akatibiwe nje ya nchi, kutokana na kuwa na uvimbe tumboni hali inayomsababishia maumivu makali na kumnyima usingizi, ombi ambalo lilikataliwa na Mahakama na kuagiza atibiwe Muhimbili.

No comments: