NA CHRISTINA MWAGALA,OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,amelishukuru Shirika la Maendeleo la Japani (JICA) kwa kukamilisha mradi wa Barabara na bustani ya Kaburi moja iliyopo mtaa wa Samora jijini hapa.
Mradi huo ambao ulianza utekelezaji wake Desemba mwaka jana na kusainiwa na Meya Mwita ambapo leo baada ya kukamilika umekabidhiwa kwa halmashauri ya manispaa ya Ilala leo (jana).
Meya Mwita alieleza kuwa mradi huo umegharimu jumla ya shilingi milioni 840 ikiwa na malengo ya kuboresha mtaa wa samora ili kuwezesha magari kutembea kwa uangalifu zaidi sambamba na kuliweka jiji kwenye muonekano mzuri.
Alisisitiza kuwa mradi huo umechukua nafasi kubwa ya maeneo ya maegesho ya magari, lakini umepelekea kuwa na muonekano mzuri kutokana na maboresho yaliyofanyika.
Hata hivyo mwakili wa JICA Nchini Tanzania Toshio Nagase alieleza kuwa mradi huo utawezesha kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Mradi huo wa barabara na bustani ya kaburi moja uliopo mtaa wa Samora, ulisainiwa na halmashauri ya jiji na hivyo kukabidhiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
No comments:
Post a Comment