Shirika lisilo la kiserikali la TGNP Mtandao limeendelea
kutoa semina kwa wakazi wa kata mbalimbali za jiji la Dar es salaam pamoja na
wanafunzi wa shule mbalimbali za jiji hilo, ikiwa ni miongoni mwa maandalizi ya
Tamasha la Jinsia.
Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika tarehe 5 – 8 mwezi 9
kwenye viwanja vya Mtandao wa jinsia TGNP, Mtandao huo umewakutanisha wanafunzi
wa shule ya msingi Umoja pamoja na Mabibo
sekondari ili kujadiliana nao mambo mbalimbali ya kwenye jamii inayowazunguka.
Akiongoza semina hiyo Mkuu wa Idara ya Utafiti na Uchambuzi
Bi. Happiness Maruchu alisema kuwa wameamua kuwapa elimu wanafunzi wa shule za
msingi na sekondari ili kuwajengea msingi mzuri wa kufahamu na kupinga vitendo
vya ukatili wa kijinsia wakiwa katika umri mdogo.
Kwenye semina hiyo walikuwa wakijadiri changamoto mbalimbali
zinazowakabiri kufikia usawa wa kijinsia.
Mila, Desturi na Tamaduni zetu zimekuwa chachu ya kuchangia
unyanyasaji wa kijinsia kwani zimeweka majukumu kwa jinsia hali inayowapa
watoto wakiume nafasi ya kutokuwa na kazi kubwa kuliko wakike. Mfano unakuta mtoto
wakiume akirudi shule anaenda kucheza mpira au anajisomea lakini mtoto wakike
anatakiwa kuosha vyombo, achote maji, kupika n.k hivyo anakosa hata muda wa
kujisomea na asipofanya vizuri shuleni analaumiwa wakati apewi muda wa
kupumzika na kujisomea kama mtoto wakiume.
Mdau wa semina za GDSS Neofita Kanumbi akichangia hoja kwenye semia iliyofanyika mapema jana makao makuu ya Mtandao wa jinsia (TGNP) |
Matabaka ni hali ya kutenganisha majukumu au fursa za
maendeleo, unakuta kuna kunakuwa na sharia kama mama anatakiwa kuwa nyumbani
kupika chakula na kufanya kazi za nyumbani na wakati baba akifanya kazi kama
zile analipwa pesa, mfano baba akipika chakula hotelini analipwa au akuwa na
toroli la maji anauza na kupata pesa lakini mama nafanya kama jukumu lake.
Kutotambulika thamani na mchango wa mwanamke - ni hali ya
kutoonekana mchango wamwanamke katika hali ya kushiriki maendeleo, hii inatokea
pale mwanamke anapotafuta mali na mumewe na baadae ndugu wanakuja kumfukuza kwa
kudai ajachangia kwa lolote kwenye upatikanaji wa mali hizo au unakuta mzazi
anaumwa na kuuguzwa na mtoto wa kike na baadae anaambiwa una haki ya kurithi
matokeo yake anapewa mali mtoto wa kiume ambaye hakuhusika na lolote kwenye kumuuguza
mzazi huyo.
Baadhi ya wanafunzi na washiriki wa semina za GDSS wakilisikiliza kwa umakini semina iliyofanyika mapema jana makao makuu ya Mtandao wa Jinsia (TGNP) |
Na wameshauri wazazi
kuwapa elimu watoto wakike kwani thamani ya mtu ipo kwenye elimu, pia binti
ataheshimika kwenye familia kutokana na elimu yake, lakini pia elimu itampa
mwanga wa kujitambua na kutambua thamani yake yeye kama mwanamke.
Kuwawezesha wanawake kiuchumi pia ni njia nzuri kwani
inayowafanya wanawake kujitambua na kutoyumbishwa na wanaume kwa ajiri ya
kipato au kuomba pesa kwa ajiri ya matumizi yake binafsi hivyo inapunguza
migogoro ya mara kwa mara kwa kuwa wote wanakuwa wazalishaji.
Mwanaharakati wa semina za GDSS Bi. Esther Tibaigaru akichangia mada kwenye semina iliyofanyika mapema jana kwenye ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo Dar es salaam |
Kuandaa mbinu za kuvunja mila potofu na mifumo kandamizi
kwenye jamii zetu kwani hii njia itatufanya tuondokane na mazoea tuliyojiwekea
ya kuwa siku zote mwanamke ni mtu wa chini na mwanaume anapaswa kukaa juu au
mtoto wa kimume anatakiwa kuwa na maamuzi
na wakike kutekeleza kinachosemwa ama kuamuliwa na mtoto wa kiume.
Lakini pia tufuate misingi ya haki za binadamu na imani za
kidini kuwa binadamu wote ni sawa na kila mmoja anatakiwa kupata haki kama
mwingine na hakuna aliye juu ya mwenzake au aliyebora zaidi ya mwenzake.
No comments:
Post a Comment