Leo ikiwa ni
tarehe 5 mwezi 8 Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) umewakutanisha wahariri wa vyombo
mbalimbali vya habari pamoja na mwanaharakati mkongwe Mama Gertrude Mungella, lengo
likiwa ni kujadili harakati za ukombozi wa wanawake kiuchumi, kijamii na
kisiasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Bi. Lilian Liundi akiongea na Wahariri wa vyombo vya habari mapema leo, kwenye Semina ilifanyika kwenye ukumbi wa mtandao huo Mabibo jijini Dar es salaam |
Lakini pia
kujadili mambo mbalimbali yanayowakabiri wanawake Kiuchumi kama kuzitafuta fursa na
namna ya kuzitumia endapo watazipata. Pamoja na sera ya serikali ya viwanda
kufahamu wanawake wamejipanga vipi kwa hili na lengo likiwa ni wanawake
kumiliki viwanda vyao na siyo kufanya kazi za kuzalisha kwenye viwanda vya
wengine.
Baadhi ya wahariri wakisiliza kwa makini wawezeshaji wa Semina iliyoandaliwa na mtandao wa jinsia TGNP Mapema leo jijini Dar es salaam |
Na pia kutakuwa
na wanawake mbalimbali ambao wamefanikiwa kuwawakilisha wenzao kwenye Nyanja mbalimbali
kama Mama Gertrude Mungella, Spika mstaafu Anna Makinda, Makamu wa Rais Samia Suluhu
n.k wakijaribu kutoa shuhuda zao walipoanza harakati mpaka kufikia mafanikio
ili kuweza kuwashawishi na wanawake wengine kuthubutu kufanya kama wao. Lakini
pia bila kusahau mchango wa wanawake waliofanya vizuri na kwa sasa wameshafariki
kama Bibi Kidude binti Baraka, Bibi Titi Mohamedi na wengine wengi.
Pia kuangali
mikataba mbalimbali ya kikanda na yakimatifa
ambayo serikali yetu imeingia ambayo inaonyesha kupinga ukatili dhidi ya
wanawake na jinsi ya kuwezesha wanawake na kiuchumi, kisiasa na kijamii kama
utekelezaji wake unafanyika ipasavyo.
Mama Gertrude Mungella akiongea na wahariri kwenye Semina iliyoandaliwa na TGNP Mtandao mapema leo jijini Dar es salaam |
Wajasiriamali toka
mikoani nao watapata nafasi ya kuja kutambulisha bidhaa zao na kujifunza jinsi
ya kupaki bidhaa zao za vyakula na nyinginezo, ili kuweza kupata soko kubwa la
ndani na hatimae kuingia kwenye ushindani wa soko la kimataifa kimataifa.
Wadau mbalimbali
toka serikalini watakuwepo kuja kuchukua mapendekezo ya wajasiriamali pamoja na
kutoa ushauri nini wafanye ili waweze kufanikiwa. Lakini pia kuzungumza na wanawake kuhusu changamoto
zinazowakabiri na namna ya kufanya utatuzi wa changamoto hizo.
Mama Gertrude Mungella akionge mbele ya kamera za waandishi wa habari kwenye semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia (TGNP) leo jijini Dar es slaam |
Kwa upande wake Mama Gertrude Mungella alipenda
kuwashauri wahariri na waandishi waliofika kwenye semina hiyo. kuweza kuwapa
nguvu wanawake kupitia vyombo vyao vya habari na siyo kuwafedhehesha hali
inayowafanya wanawake wengi kujiona wao ni watu wa chini. Hali inayowafanya
wanawake wengi kujiona hawawezi kufanya mambo makubwa katika jamii yao.
Lakini pia
alipenda kuwashauri TGNP na wadau wengine wote juu ya matumizi mazuri ya vyombo
vya habari “media ukizitumia vizuri zinaweza kukufikisha pazuri lakini
ukishindwa kuzitumia pia zitaharibu malengo na kile ulichokikusudia na baadae
utalaumu wamekuandika vibaya hali ambayo siyo nzuri”.alisema Mama Mungella
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mtandao wa jinsia |
Na mwisho alipongeza
jitihada zinazofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania kuwa kuendeleza harakati za
ukombozi wa mwanamke, kwani bila wao mambo mengi yangesahaulika na hata wao
waliojenga historia wasingeendelea kujulikana kama sio kuitwa kwenye shughuli
kama hizi.
No comments:
Post a Comment