Wednesday, August 30, 2017

SASA INAWEZEKANA KUWEKA VITUO VINGI VYA KUSIMAMA UNAPO TUMIA PROGRAMU YA UBER

Kampuni ya Uber nchini Tanzania imezindua zana mpya kwenye programu yake ya Uber inayowapa wasafiri nyenzo za kuweka vituo vingi vya kusimama wanapokuwa safarini. Tafsiri yake ni kwamba kipengele hiki kinawarahisishia wasafiri utaratibu wa kuweka vituo vingine vya kusimama wanaposafari kwa wakitumia mfumo wa Uber.  
Akizungumzia maboresho haya, Meneja Msimamizi wa Uber Nchini Tanzania, Bw. Alfred Msemo amenukuliwa akisema “Programu hii inawaondolea wasafiri na madereva kero ya kubadilisha mahali wanakoenda mara kwa mara, hususan inapotokea kwamba safari ina vituo vingi vya kusimama. Sambamba na kuwasaidia madereva ambao hawana uwezo wa kubadilisha vituo vya kusimama, maboresho haya yanasaidia katika mchakato wa kuendelea na safari kwa sababu vituo hivi vitakuwa ni mwendelezo wa safari.” Mwisho wa Nukuu.
Wasafiri wanaombwa kuingia katika akaunti zao za Uber ili waweze kutumia zana hii na kuita gari. Kupitia kwa zana hii sasa wasafiri wanaweza kugusa alama ya “+” iliyo karibu na kisanduku cha mahali anakoenda “Ungependa kwenda Wapi” ili waongeze kituo kingine cha kusimama wakati wowote wanapokuwa safarini. Kadhalika wasafiri wanaweza kuongeza au kuondoa kituo cha kusimama wakiwa safarini. Kufanikisha hili, wasafiri wanatakiwa kuongeza, kubadilisha, au kuondoa mahali wanakoenda kwenye skrini ya safari iliyo kwenye programu ya Uber.
Kipengele hiki kimetusaidia kurahisisha utaratibu wa kushukisha wasafiri njiani. Ima unaenda kwenye mtoko na ungependa kuwachukua marafiki zako njiani ukielekea katika uwanja wa ndege, au unarudi nyumbani baada ya shughuli zako mjini na ungependa marafiki zako washuke njiani, sasa haya yote yako kiganjani mwako,” amesema Bw. Mr. Msemo.
Jinsi ya kutumia kipengele hikii:
Screen Shot 2017-08-21 at 4.35.11 PM.png

No comments: