LEO tarehe 12/08/2017 mataifa mbali mbali duniani yanaadhimisha kilele cha siku ya
vijana duniani.Ni zaidi ya miaka 18 sasa tangu umoja wa mataifa uitangaze siku
ya August 12 kuwa ni siku maalum ya vijana duniani
.Umuhimu wa vijana katika
maendeleo endelevu ya mataifa ndio chanzo kikuu cha kutambulika rasmi kwa siku
hii muhimu.
Vijana wa ACT-WAZALENDO
tunaungana na vijana wenzetu wote Duniani katika kuazimisha siku hii muhimu yenye
kauli mbiu ‘VIJANA NI SEHEMU YA KUTENGENEZA NA KULINDA AMANI’ Sisi sote ni
mashahidi na wahubiri wa kauli mbiu hii kwa kuwa tunafahamu hakuna maengeleo
endelevu yatakayopatikana bili ya Amani na usalama.Kwa kutambua umuhimu wa siku
hii kwa vijana,Ngome ya vijana
ACT-WAZALENDO tunatambua Vijana kuwa sehemu ya kutengeneza Amani na
usalama, ni matokeo ya vichocheo vya mambo mengi yatakavyowafanya vijana
washiriki katika kutengeneza Amani na usalama wa nchi yetu.
Tunaamini Uhuru wa vijana
kujieleza, ushirikishwaji wa vijana katika maamuzi pamoja upatikanaji wa Ajira
kwa vijana, ni miongoni mwa mambo muhimu yatakayotupelekea vijana tuwe sehemu
ya kutengeneza Amani na usalama wa nchi yetu.
Vijana wa
ACT-WAZALENDO,Tunaitaka serikali kwa kutambua mchango wa vijana katika
kutengeneza Amani na usalama wa taifa letu,ichukuwe jitihada za dhati za
kuhakikisha inatengeneza mazingira rafiki kwa vijana kuendelea kuwa kizazi
chenye uhuru wa kujieleza na kuhoji mambo ya msingi katika taifa letu.Kufanya
hivi ,si kama kutalisaidia taifa kuwa na viongozi wazuri na wazalendo katika
ofisi zetu,bali litaamsha hali ya wahojiwa na wakosolewa kujitathimini na
kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa.Tunasema haya kwa kutambua namna vijana
tunavyonyimwa fursa ya kushiriki katika majukwaa ya kusikiliza na kujieleza kwa
kile kinachoitwa marufuku ya mikutano ya kisiasa kwa wasiokuwa viongozi
wamaeneo husika.Vijana tusiokuwa wabunge wala madiwani,Hatuna hatuna nafasi ya
kujifuza siasa za majukwaani kwa vitendo kwa sasa.
Jambo lingine muhimu ambalo
ni kichocheo cha vijana kuwa sehemu ya kutengeneza Amani na usalama wa taifa
letu ni Ajira,Agenda hii ya ajira kwa vijana imekuwa ni tatizo sugu na
tumewasikia viongozi wetu wakiendelea kulisemea kila siku.Vijana wa
ACT-WAZALENDO hatutaki tena kuliongelea suala hili kisisa kwa kuwa tunajua ni
namna gani maelfu ya vijana waliomaliza vyuo vikuu hawajafanikiwa kupata ajira
kutokana na mazingira halisi ya ufumo wa ajira za serikalini ambazo ndio
zinategemewa na vijana wengi.Tunajua serikali imeshindwa na haina uwezo wa
kuwaajiri vijana wote wanaomaliza elimu katika ngazi mbalimbali kwa sababu
nyingi tunazoelezwa kikiwa pamoja na sababu za kibajeti.
Kwa masikitiko
makubwa,hata sekta binafsi ambayo tulianza kuiona kama mkombozi kwa vijana
wengi kuajiriwa huko,nayo imeanza kupunguza wafanyakazi kwa kasi ya ajabu kwa
sababu mbalimbali ikiwemo za serikali kutoa kauli na misimamo ya kikodi na
mengineyo bila kuwapa wafanyabiashara muda wa maandalizi wa kutosha.Sote
tunakumbuka sakata la vituo vya kuuza mafuta na maamuzi ya serikali ya matumizi
ya EFD.Ni idadi kubwa ya vijana walipoteza ajira zao za kuhudumia vituo vya
mafuta na kuishi bila Amani kwa kipindi cha maamuzi haya.Vijana wa
ACT-WAZALENDO tunaishauri serikali kufanya tathimini za kina pale wanapotaka
kufanya maamuzi yanayohusu sekta binafsi ili walau kuepusha mihangaiko na
mataso kwa vijana walioajiriwa katika sekta binafsi.
Kwa kutambua ukubwa wa
tatizo la ajira kwa vijana wa kitanzania,sisi vijana wa ACT-WAZALENDO,Leo hii
tunaanzisha rasmi kampeni ya kuwahamasisha vijana wenzetu kuingia rasmi katika
Kilimo.Kampeni hii tumeipa jina ‘TUAMUE SASA,KILIMO NI AJIRA’.Serikali
imeshindwa kutuajiri maofisini,Twendeni shambani tukalime ,Tuzalishe malighafi
,tukiwa matajiri wa malighafi,matajiri wenye viwanda tunavyoambiwa vinaletwa
,watatutafuta wenyewe.Tunawahamasisha vijana kuungana na kwa pamoja kujiandaa
kupitia fursa zilizopo katika maeneo yetu kuzalisha mali shambani.
Ngome ya vijana ya ACT
WAZALENDO,Inawataka vijana wote nchini kuacha kulia na ajira za serikalini
ambazo hazipo.Tuamue sasa,kilimo kukikimbilia.Mashambani twendeni,mali
tukazalishe.Hii ndio namna pekee ya kujikomboa kutoka kwenye kilio kikuu cha
ajira.Kampeni hii itakayoongozwa na Vijana wa ACT WAZALENDO itapita kwenye
mikoa yote inayozalisha mazao ya chakula na biashara ,Kukutana na vijana
kuwahamasisha kushiriki katika kilimo kutokana na mazingira waliyopo.Tutaenda
TABORA kuwataka vijana waione Tumbaku ndio muokozi wao,Tanga Katani,Tutawaambia
vijana wa kusini Korosho ndi ajira yao,Tutawaambia vijana wa Mbeya wajiandae na
vitalu vya Mpunga.Vijana wa Singida na Dodoma wajiandae na Alizeti ili
wanyeviwanda vya mafuta wawatafute.Tutawafikia vijana wa maeneo yote ya
Tanzania.’TUMEAMUA SASA,KILIMO NI AJIRA’
Chama chetu kinaamnini
katika siasa za maendeleo,Sisi vijana wa chama tumeamua sasa kuhamasisha
maendeleo endelevu ya vijana wa Tanzania kupitia kilimo,Ili waweze kuwa sehemu
ya kutengeneza Amani na usalama wa nchi yetu.
Mwisho tunazitaka sekta
zote zinazoambatana na Kilimo zitengeneze mazingira rafiki ya kuwasapoti vijana
katika shughuli za kilimo ikiwa pamoja na kuwapatia taarifa za fursa za
kuwaendeleza vijana katika kilimo zinazopatikana katika taasisi zao kwa wakati
sahihi.Tunatoa wito wa Sera za taasisi za fedha na mashirika yanayojihusisha na
kilimo kupitiwa upya ili ziweze kuwasaidia vijana katika shughuli za
kilimo.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU TUBARIKI VIJANA WA TANZANIA.
Asanteni
LIKAPO B,LIKAPO
Mratibu Vijana Taifa
ACT-WAZALENDO
No comments:
Post a Comment