Wednesday, August 30, 2017

VIDEO ANGALIA YALIYOJIRI KWENYE RIPOTI YA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU

Leo ikiwa ni tarehe 30 ya mwezi agosti mwaka 2017 kituo cha sharia na haki za binadamu kimezindua ripoti yake ya biashara ya mwaka 2016 iliyofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo uliudhuriwa na wadau mbalimbali toka taasisi binafsi na serikalini lengo likiwa ni kupata elimu juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye sekta ya viwanda na makampuni mengi hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Bi. Helen Kijobisimba akikata utepe wakati akizindua Ripoti ya Biashara ya 2016 katika hotel ya Protea Courtyard mapema leo jijini Dar es salaaam.
Akiwasirisha ripoti hiyo mwanasheria wa Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu Bw. Pasiasi Mloe alisema utafiti huo umefanyika katika mikoa 14 ya hapa nchi kwenye viwanda na makampuni mbalimbali.

Miongoni mwa vitu hivyo ni baadhi ya wafanyakazi wa viwandani na kwenye baadhi ya makampuni kutokuwa na mikataba ya kazi, au mikataba inakuwepo na badala yake anabaki nayo muajiri hali inayofanya wafanyakazi kukosa haki kwenye maeneo yao ya kazi.
Mwanasheria wa Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu Bw. Pasiasi Mloe akiwasirisha ripoti hiyo mbele ya meza kuu pamoja na wageni waalikwa kwenye tafrija iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam
Lakini pia baadhi ya makampuni kutokuwepo na vyama vya wafanyakazi hali inayofanya wafanyakazi kukosa utetezi pale muajiri anapokwenda kinyume na makubaliano, au vyama vinakuwepo lakini vinasimamiwa na waajiri hali inyofanya waajiriwa kushindwa kupata ututezi wowote.

Aidha bwana mloe alisisitiza kuwa wafanyakazi walio wengi kwenye viwanda na makampuni hayo hawajui umuhimu wa mifuko ya hifadhi kuwa inaweza kuwasaidia pale wanapopata tatizo wakiwa kazini hali inayofanya kukosa fidia zao pale wanapopata kilema cha kudumu au tatizo lolote linalofanya wasiweze kufanya kazi tena.
Wafanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu.
Lakini pia tatizo lingine ni kwa upande wa usawa wa kijinsia  kwani makampuni mengi yamesema kuwa hayapendi kuajiri wanawake kwenye kampuni zao kwani hawaamini kama wanaweza kufanya kazi sawa na wanaume, na ndio sababu kwenye viwanda vingi wameajiriwa wanaume wengi na wanawake wapo wachache.

Na kitu kingine wamejaribu kuangalia wakazi wa karibu na migodi pamoja na viwanda je wananufaika vipi na rasirimali hizo kwa kuwa karibu nazo, ikiwa ni kupata ajira na huduma nyinginezo za msingi.



                                            click hapa kuangalia tukiozima lilivyokuwa..

                       

No comments: